The House of Favourite Newspapers

Baba Rihanna Amkataa Mpenzi wa Mwanaye!

0
Mzee Fenty akiwa na mkewe

SIMTAKI! Huku mwanamuziki mwenye jina kubwa, RihannaRiRi‘ akiwa amemtangaza bilionea mkubwa, Hassan Jameel kama mpenzi wake mpya, mzazi wa mrembo huyo, Ronald Fenty ameibuka na kusema kwamba hakubaliani kabisa na uamuzi wa mtoto wake kuwa na mshikaji huyo.

Mtu aliye karibu kabisa na familia hiyo alisema kwamba mzee Fenty alishtuka baada ya kuona mtoto wake akianza kutoka kimapenzi na Mwarabu huyo kitu ambacho aliona kuwa si sahihi.

Rihanna akiwa na Jameel

“Siku zote baba yake Rihanna amekuwa akitamani kumuona mtoto wake akitoka kimapenzi na mtu mweusi lakini si Mzungu au Mwarabu. Amekasirishwa na uamuzi wa binti yake,” kilisema chanzo hicho.

Pamoja na mzazi wake kuonyesha kummaindi lakini Rihanna hakuzungumza kitu chochote kile kwani anachokiamini ni kwamba mtu anaweza kumpenda mtu yeyote yule na si kuangalia ngozi wa utaifa.

Na: Nyemo Chilongani, (GPL)

Leave A Reply