The House of Favourite Newspapers

Baba Samatta Afichua Alichoelezwa na Grealish Villa

0

BABA mzazi wa mshambuliaji wa Aston Villa, Mtanzania, Mbwana Samatta, mzee Ally Samatta amefunguka kuwa amefanikiwa kuzungumza na nahodha wa timu hiyo Jack Grealish baada ya kukutana naye mara baada ya mchezo wa fainali ya Carabao Cup uliopigwa wikiendi iliyopita.

 

Mzee Samatta alikuwa ni miongoni mwa Watanzania wachache walioweza kushuhudia mchezo huo wa fainali wakiwa kwenye Uwanja Wembley uliopo katika Jiji la London huku Aston Villa ikipoteza kwa kipigo cha mabao 2-1, Samatta akifunga bao la kufutia machozi kwa Villa.

BABA mzazi wa mshambuliaji wa Aston Villa, Mtanzania, Mbwana Samatta, mzee Ally Samatta

Akizungumza na Championi Jumamosi mara baada ya kurejea nchini kutoka Uingereza, mzee Samatta alisema kuwa alipata bahati ya kuzungumza na nahodha wa timu hiyo, Grealish ambaye amekuwa akifurahishwa na kiwango kinachoonyesha na Samatta katika timu hiyo kwa sasa, kitu ambacho hata yeye kimemshangaza.

 

“Nilikutana na wachezaji wengi kwa sababu watu walikuwa ni wengi lakini hata yule Grealish, tulionana na tukazungumza, kikubwa alichokisema ni kumpongeza Samatta kwa jinsi anavyoonyesha uwezo mkubwa uwanjani na anaamini atawasaidia kuweza kubaki katika Premier League.

“Lakini sikutaka kumueleza kwamba amekuwa akimnyima pasi kama ambayo imekuwa ikiandikwa mitandaoni, ila ni mchezaji anayeonyesha kwamba ni muungwana.

 

“Pia Marvelous Nakamba nilizungumza naye, alionyesha kufurahia kuniona pale na ameniahidi kwamba watapambana kuhakikisha Villa haishuki kwa sababu Samatta amekuwa akionyesha ubora wake ndani ya uwanja, hata baada ya chakula cha jioni wawili hao (Mbwana na Nakamba) waliondoka pamoja,” alisema mzee Samatta.

KUELEKEA SIMBA VS YANGA: MASHABIKI Watunishiana Misuli ” MSIJE na Matokeo Yenu”


 

Leave A Reply