The House of Favourite Newspapers

Baba Yake na Msuva Aitaja Timu Anayoelekea Mtoto Wake Algeria

0
Simon Msuva

 

RASMI sasa kiungo Simon Msuva anakwenda kukipiga klabu ya CR Belouizdad ambao ni Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu ya Algeria na suala la muda yeye kwenda kusajiliwa huko.

Hiyo ni baada ya tetesi kuzagaa za kiungo huyo kuwepo katika mazungumzo na Simba wanaotajwa kuiwinda saini yake katika msimu huu kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kiungo huyo hivi karibuni alitajwa, pia kuwepo katika mazungumzo na Yanga katika vipindi tofauti vya usajili ikiwemo katika usajili huu mkubwa unaotarajiwa kufungwa Agosti 31, mwaka huu.

Taarifa ambazo imezipata Championi Jumatano, kutoka Simba juzi Jumatatu walikutana na kiungo huyo kwa ajili ya mazungumzo ambayo hayakufikiwa muafaka kutokana na ofa ya Sh 750Mil aliyoitaka kuonekana ni mzigo mkubwa kwa klabu hiyo na sasa ameelekeza akili zake klabu ya CR Belouizdad.

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa, kiungo huyo ana ofa mbili kutoka Algeria zinazofikia zaidi ya Sh 1.8Bil ambazo ni klabu ya CR Belouizdad yenye nafasi kubwa ya kumsajili na USM Algers iliyocheza Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Yanga.

Baba mzazi wa kiungo mshambuliaji wa Difaa El Jadida, Simon Msuva, Mzee Happygod Msuva

Aliongeza kuwa kiungo huyo mwishoni mwa wiki hii anatarajiwa kupanda ndege kwenda Algeria kukamilisha dili lake la usajili klabu ya CR Belouizdad iliyoweka mzigo mkubwa wa fedha.

“Hizo zinazoendelea ni taarifa za mitandaoni pekee, kwani Msuva hana mpango kabisa wa kusaini moja ya klabu hizo kubwa za Simba na Yanga, kwani yeye mipango yake yote ni kucheza soka nje ya nchi.

“Tayari ana ofa mbili kubwa kutoka Algeria ambazo ni USM Algers na Cr Belouizdad ambayo yenyewe ndio uhakika imemalizana naye kwa asilimia kubwa, kilichobakia ni yeye kwenda kumalizana dili hilo kwa kusaini.

“Simba na Yanga hazina pesa ya kumpa Msuva, ni kutokana na ofa nzuri aliyowekewa huko Algeria, hivyo hatasajiliwa na timu yoyote ya hapa nyumbani,” alisema mtoa taarifa huyo.

Baba wa kiungo huyo, Happygod Msuva alipotafutwa na Championi Jumatano kuzungumzia hilo alisema kuwa: “Kwa sasa Simba na Yanga wasahau kumsajili Msuva, kwani malengo yake ni kucheza soka la kulipwa nje ya nchi na sio hapa.

“Nisingependa kulizungumzia hilo kwa sasa hivi, yeye mwenyewe ndio anaweza kuliweka wazi ikiwemo ofa alizowekewa mezani,” alisema Baba Msuva

STORI NA WILBERT MOLANDI NA IBRAHIM MUSSA

Leave A Reply