The House of Favourite Newspapers

Babu Seya, Papii Kutoka Jela

0

jeshi11 (1)Nguza Viking “Babu Seya’ (wa pili kulia) na mwanaye Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ (wa tatu kulia) wakisindikizwa na askari magereza.

Elvan Stambuli, RISASI

DAR ES SALAAM: Mrithi wa kazi ya utabiri za marehemu Sheikh Yahya Hussein, Maalim Hassan Yahya Hussein amesema mwanamuziki aliyefungwa jela maisha, Nguza Viking “Babu Seya’ na mwanaye Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ watatoka jela kama alivyowahi kutabiri baba yake.

yahyaMarehemu Shekhe Yahya.

MAALIM HASSAN AIBUA MAZITO

Akizungumza na gazeti hili juzi, Maalim Hassan alisema baba yake aliwahi kutabiri kuwa mwanamuziki huyo na mwanaye Papii watatoka jela licha ya kufungwa maisha jela, naye ameona kuwa utabiri huo bado upo palepale.

“Unajua tabiri inapofanyika siyo lazima itimie siku ileile au mwaka uleule, unaweza kudumu kwa miaka hata hamsini lakini ipo siku hutimia na watu kuukumbuka, “ alisema Maalim Hassan.

babuseyarufaa1

WATU HUWAULIZIA

Akaongeza: “Watu wengi wamekuwa wakiniulizia juu ya utabiri wa marehemu Sheikh Yahya kuhusu Babu Seya, jibu ni hili kwamba ipo siku wataachiwa na watu watakuja kushangazwa kwani subira yavuta kheri.”

shekhe yahya hussen

Maalim Hassan Yahya Hussein.


KESI MAHAKAMA YA AFRIKA

Kesi ya Babu Seya na mwanaye hivi sasa ipo katika Mahakama ya Haki za Binadamu Afrika na juzi Jumatatu majaji walitarajia kupitia maombi ya rufaa za kesi mbalimbali ikiwemo ya wanamuziki hao.

MARANDOJAJI RAMADHANI ALONGA

Taarifa iliyotolewa Jumatatu iliyopita na  Rais wa Mahakama ya Afrika, Jaji Augustino Ramadhani, ilisema kuwa majaji wa mahakama hiyo watapitia maombi ya wanamuziki hao katika kikao cha faragha na kama yatafaa, itapangwa tarehe kuanza kusikilizwa kwa shauri lao.

Mahakama hiyo ina majaji 11 kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Afrika na hukutana mara nne kwa mwaka katika vikao vyake vya kawaida.

babuseyarufaa2WANACHOKIOMBA KORTINI

Babu Seya na mwanaye katika shauri hilo namba 006/015 wanaiomba mahakama ya Afrika kutoa uamuzi kuwa haki zao zilivunjwa na hivyo waachiwe huru na kulipwa fidia.

Moja ya hoja walizopeleka katika mahakama hiyo, wanamuziki hao wamedai kuwa mwenendo wa shauri lao haukufanyika kwa kuzingatia sheria, katika hatua zote walikuwa wakitetewa na wakili maarufu, Wakili wa Mahakama Kuu, Mabere Nyaucho Marando.

ALICHOSEMA SHEIKH YAHYA

Akizungumzia utabiri wake dhidi ya hukumu iliyotolewa katika Mahakama ya Rufani jijini Dar es Salaam, Shekh Yahya alisema, alijua wazi kwamba tatizo hilo lingetokea lakini alidai kuwa lilitokana na sababu za kimila (za akina Babu Seya), lakini akasema ipo siku watakuwa huru hata kama watachelewa kutoka.

MAMBO ALIYOPUUZA BABU SEYA

Alisema, alichokuwa akikiona ni upuuzwaji wa matambiko, kisomo au dua za kikwao, zilizotakiwa kufanywa na Babu Seya zamani, ndiyo maana sasa wanapata mateso sasa huko gerezani.

Alisema, Babu Seya anatoka katika ukoo wa kifalme ambao hutumia jina la Mbangu, lakini kuna mambo muhimu kufuatana na familia na mila za kabila lao, ambayo Babu Seya alitakiwa kuyakamilisha zamani, lakini hakufanya hivyo.

 

WASIA WAKE

Aliwataka watoto wa Babu Seya waliokuwa wameachiwa huru na mahakama, Mbangu na Francis Nguza Viking kumuombea baba yao na siyo kumuombea yeye tu bali pia kujiombea wote pamoja.

”Mnapaswa kumfanyia sadaka, msome kisomo kabla hajatoka, kwa mila za kwenu. Msije mkasema labda tatizo ni dansi, maana kama ni dansi mmeanza kuimba miaka mingi kabla, ila tatizo ni hilo la kusahau au kupuuza mila,” aliasa Sheikh Yahya wakati huo.

Aidha mtabiri huyo aliwapatia vijana hao fedha kiasi cha shilingi laki moja kwa ajili ya kuwasaidia katika mahitaji yao.

 

KUMBUKUMBU

Juni 25, 2004, Babu Seya na wanaye, walihukumiwa kifungo cha maisha jela, baada ya kukutwa na hatia ya kuwaingilia kimwili watoto wadogo kumi wa Shule ya Msingi Mashujaa iliyopo Sinza, jijini Dar es Salaam, hata hivyo katika Mahakama ya Rufaa Tanzania wanaye wawili Nguza na Francis waliachiwa huru kwa kutokutwa na hatia.

Leave A Reply