The House of Favourite Newspapers

Babu wa Darasa la Kwanza Ashangaza Wengi

Kikongwe Nyamohanga Suguta wa pili (kulia)

MARA: KIKONGWE Nyamohanga Suguta (75) wa Kitongoji cha Kibeyo, Kijiji cha Getenga Kata ya Mbogi wilayani Tarime mkoani hapa, ameshangaza watu wanaomzunguka katika kufuatia uamuzi wake wa kuanza darasa la kwanza mwaka huu katika Shule ya Msingi Makerero, Uwazi limezungumza naye.

Mzee Suguta alisema kuwa, alifikia hatua hiyo baada ya kuwiwa na elimu muda mrefu kwa sababu alikomea darasa la pili mwaka 1950 katika Shule ya Msingi ya Nyamaranya nchini Kenya kutokana na kukumbwa na changamoto kadhaa.

…akiangalia mifugo yake..

KWA NINI AMEAMUA KUREJEA DARASANI?

“Sababu hasa iliyonifaya nirejee shule, ni baada ya kugundua muda wote nilipata hasara ya kurejesha chenji pale nilipowauzia ndizi za shambani kwangu wateja. Nimekuwa nikijikuta nawapa chenji zote bila kujua namna ya kukata mauzo yangu.”

 

 

Akiwa darasani

KUMBE ENEO LA SHULE ALILITOA YEYEMzee Suguta pamoja na kuonesha mfano huo, familia yake ndiyo iliyotoa ardhi na kujengwa shule hiyo na kuwafanya wanafunzi kuwa karibu tofauti na awali walikuwa wakitembea umbali mrefu katika Shule ya Msingi ya Kitakutiti. “Kwanza wakati nahitaji kuanza shule nilishindwa baada ya kuona umbali uliopo, ndiyo maana mimi pamoja na ndugu zangu, Simon na Mwikabe tulitoa eneo la ardhi kulikojengwa shule hii ili kuwa karibu na nilianza chekechea mwaka jana, 2016 na mwalimu wangu aliyeniwezesha kufanya vyema katika mtihani wangu wa kuingia darasa la

kwanza ni Margaret,” alisema denti huyo.

MWALIMU WAKE WA DARASA LA AWALI

Margaret Albinus ni mwalimu wake wa darasa la utayari ambapo alikuwa na haya: “Mzee huyo ana bidii sana, alianza kimchezomchezo, alihudhuria muda wote mwaka mzima na alipokosa kuja shule ni kwa sababu ya kupatwa na shida kubwa na aliomba ruhusa. “Alifanya vyema katika masomo yake, kusoma, kuandika na mahesabu na muda wote alitii. Ni msikivu hata pale nilipoagiza wanafunzi wenzake wafanye usafi wa mazingira naye alifanya. Nilimuonea huruma kufanya kazi hizo badala yake nilimpati ukiranja”

…aikiingia nyumbani kwake…

MWALIMU MKUU SASA Naye mwalimu  mkuu wa shule hiyo iliyofunguliwa mapema mwaka huu, Riziki Focus, alisema kuwa mzee huyo aliandikishwa katika mfumo usio rasmi. “Mzee Suguta ni mwanafunzi wa darasa la kwanza katika mfumo usio rasmi, yaani Memkwa na tunamchanganya na watoto wadogo kutokana na kutokuwepo kwa darasa la watu wazima. “Darasani yuko vizuri sana, ni msikivu na mtiifu, mwenye nidhamu sana maana mimi unayeniona hapa ni sawa na binti yake, lakini ananitii na kunipa heshima zote kama mwalimu wake mkuu wa shule,” alisema mwalimu Riziki.

MWENYEKITI WA KITONGOJI ANAMZUNGUMZIAJE?

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kibeyo, Meshack Jushuo ‘Chui’: “Mzee alichokifanya ni kizuri na ni mfano wa kuonesha kuwa, Elimu Haina Mwisho, wengine wanamcheka lakini pia ni kuiambia jamii na serikali kwa pamoja kwamba, watu wanaopenda kujiendeleza wapo na hata kwa njia ya Qualify Test (QT) na enzi za nyuma kulikuwa na Masomo ya Elimu kwa Njia ya Posta (Correspondence Adult Education), lakini leo hii wamerudi nyuma wakati Wakenya wenzentu wanasonga mbele.” Uwazi lilimshuhudia mzee huyo akitoka shuleni kurejea nyumbani kwake, akiwa ameongozana na wanafunzi wengine huku akiwahi kwa madai kwamba ana

Comments are closed.