The House of Favourite Newspapers

#BadNews: Watu 10 Wafariki kwa Ajali ya Ndege

WATU 10 wameripotiwa kupoteza maisha katika Jimbo la Texas baada ya kutokea kwa ajali ya ndege binafsi aina ya Beechcraft Super King Air 350, katika eneo la Uwanja wa Ndege katika Manispaa ya Addison nchini Marekani.

 

Taarifa zinaeleza kuwa ndege hiyo ilipoteza mwelekeo wakati ikiruka na baadaye kuanguka na kuwaka moto.

 

Watu saba kati ya watu 10 waliofariki walitambuliwa jana Jumatatu huku kifaa cha kurekodi ya sauti kutoka kwenye ndege kikipatikana.

Mpaka sasa Mamlaka ya Anga nchini humo haijatoa sababu ya ajali hiyo iliyotokea juzi Jumapili asubuhi, na uchunguzi unaendelea. Timu ya watalaam watano wapo eneo la tukio kufanya uchunguzi na kwamba ripoti kamili itatolewa wiki ijayo.

Kati ya waliofariki, watu wawili walikuwa ni wafanyakazi wa ndege hiyo huku wanane wakiwa ni abiria ambao miongoni mwao, wanne ni ndugu wa familia moja.

Ndege hiyo ilikuwa imepangiwa kuondoka Addison, umbali wa maili 15 Kaskanizi mwa Dallas kwenda St. Petersburg, Florida.

Comments are closed.