The House of Favourite Newspapers

Bahati Nasibu Ya Shinda Gari, Wasomaji Kawe Wamiminika Kujaza Kuponi

0
Ofisa Masoko wa Global Publishers, Songoro Bilal (kulia) akiwafafanulia jambo wasomaji wa gazeti la Championi kuhusiana na Bahati nasibu ya shinda gari inayopatikana ndani ya gazeti hilo.
Msoamaji akijaza kuponi yake kushiriki bahati nasibu ya shinda gari.
Ofisa Masoko wa Global Publishers, Songoro Bilal (katikati) akiwashuhudia wasomaji wakijaza kuponi.
Msomaji wa Championi akiweka kuponi yake kushiriki bahati nasibu.
Mmoja wa wasomaji wa magazeti ya Championi na SpotiXtra akionesha kuponi ya kushiriki bahati nasibu ya shinda gari.
Wasomaji wa Gazeti la Championi wakijaza kuponi kushiriki bahati nasibu ya shinda gari.
… Bilal (kulia) akiwafafanulia jambo wasomaji wa gazeti la Championi kuhusiana na Bahati nasibu ya shinda gari inayopatikana ndani ya gazeti hilo baada ya mmoja wa wasomaji kukata kuponi.

 

 

Wasomaji mbalimbali wa magazeti ya Championi na Spoti Xtra wa maeneo ya Kawe, Mikocheni hadi Msasani mapema leo wamemiminika kujaza kuponi kwa ajili ya kushiriki droo ya Bahati nasibu ya Shinda gari  iliyopewa jina la Chomoka na Gari Mpya  inapatikana kupitia magazeti hayo yanayochapishwa na Kampuni ya Global Publishers.

 

 

Timu ya maofisa masoko wa Publishers walitembelea maeneo hayo na kushuhudia umati wa watu wakijaza kuponi na kwa ajili ya kuingia katika droo ya bahati nasibu hiyo ambayo mshindi atanyakua ndinga mpya aina ya FunCargo.

 

 

Akipiga stori na wasomaji hao Ofisa Masoko wa Global Publishers, Anthony Adam,  amewasisitiza wananchi hao kununua kwa wingi magazeti ya Championi na Spoti Xtra ili waweze kuwa miongoni mwa washindi wataoinyakua ndinga hiyo.

 

‘Niwasihi wakazi wa Kawe na maeneo mengine muendelee kununua magazeti yetu ili muwe miongoni mwa washindi, tutatoa gari mpya siku ya mwisho ya droo na kabla ya droo kubwa wapo ambao kila wiki watakuwa wanajinyakulia simu mpya za kijanja, Smart Kitochi, ambazo ndani yake kutakuwa na bando la bure na APP ya Global Radio.

 

JINSI YA KUTUMA:

Mpe kuponi yako muuza magazeti aliye karibu nawe popote ulipo, au peleka kwenye Ofisi za Global Publishers zilizopo Sinza-Mori, Dar, au tuma kwa njia ya barua, Jishindie GariGlobal PublishersS.L.P 7534, Dar es Salaam.

Kwa maelezo zaidi, piga simu no: 0717 020792 au 0672 324759.

 

MASHARTI YA KUSHIRIKI:

Wafanyakazi wa Kampuni ya Global Publishers & General Enterprises Ltd na watoto chini ya miaka 18 hawaruhusiwi kushiriki bahati nasibu hii.

 

Kuponi zitumwe kutoka nakala halisi ya gazeti, vivuli (fotokopi) haviruhusiwi. Mtu anaruhusiwa kutuma kuponi nyingi kadiri awezavyo ili ajiongezee nafasi ya kushinda. Kuponi zote zitachezeshwa kwenye droo ya awamu ya kwanza, ya pili na ya tatu.

Leave A Reply