The House of Favourite Newspapers

Bajeti: Serikali Yafuta Ushuru wa Gesti, Yapiga Pini Usafirishaji wa Madini

0
DODOMA
 
Serikali imetangaza kufuta ushuru wa huduma kwenye nyumba za kulala wageni. Hayo yameelezwa leo (Alhamisi) bungeni na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Phillip Mpango wakati akiwasilisha bajeti kuu ya mwaka 2017/18.
Pamoja na ushuru huo, pia Serikali imefuta ushuru wa mabango yanayoelekeza mahali zinapopatikana huduma za kijamii kama vile shule na hospitali.
Katika hatua nyingine, Serikali imetangaza neema kwa wafanyabiashara wadogo wadogo wasio rasmi wakiwamo mama lishe na baba lishe, ikiahidi kuwapa vitambulisho maalumu vitavyosaidia kuwatambua rasmi.
Amesema vitambulisho hivyo vitawasaidia kutengewa maeneo maalumu ya kufanyia biashara.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango amesema hatua hiyo inalenga kuwasaidia wafanyabiashara hao ili kukuza mitaji yao.
Serikali pia imesema haitaruhusu usafirishaji wa madini moja kwa moja kutoka mgodini na kupelekwa nje ya nchi.
Hayo yameelezwa leo Alhamisi na Waziri wa Fedha na Mipango, Phillip Mpango wakati akiwasilisha hotuba ya bajeti kwa mwaka 2017/18.
Badala yake kutakuwa na viwanja maalumu vya kimataifa katika bandari, migodini na madini hayo yatathibitishwa na kupewa kibali kabla ya kusafirishwa nje.
“Kibali hicho kitatozwa ada ya asilimia moja ya thamani ya madini hayo,” amesema.
Amesema Serikali itatangaza rasmi tarehe rasmi ya kuanza kwa ada hiyo.

LIVE Kutoka Bungeni, Uwasilishwaji wa Bajeti Kuu ya Serikali 2017/2018

Leave A Reply