The House of Favourite Newspapers

BAKITA Kufanya Uhariri wa Mashairi Bure kwa Wanamuziki wa Dansi

0
Nyoshi el Saadat

BARAZA la Kiswahi Tanzania (BAKITA) limeamua kuongeza nguvu katika kuunganisha muziki wa dansi hapa nchini kwa kuwakaribisha wanamuziki wote kwa ajili ya kupeleka mashairi ili kufanyiwa uhariri bure.

 

Wanamuziki hao wameungana kwa kuja na Tamasha la Tanzania All Stars, litakalofanyila katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, Desemba 9 mwaka huu, tamasha lililopewa jina la Umoja na Uzalendo.

 

Akizungumza Mratibu wa maandalizi ya tamasha hilo Juma Mbizo, amesema kuwa, tamasha hilo litaanza saa 4:00 asubuhi hadi saa 4:00 usiku, ambapo limewaalika wasanii mbalimbali wa muziki huo wa Dansi.

Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA)

Mbali na Wanamuziki wa Dansi pia wamewaalika wasanii wa muziki wa Bongo Fleva na Singeli ili wakaone na kujifunza mengi kutoka kwa wasanii wakongwe.

 

“Mbali na tamasha la Umoja na Uzalendo, pia tumetoa albam yenye nyimbo 7, ambapo wameshiriki wakongwe Mbalimbali.

 

“Katika albam ya Tanzania All Stars ambayo imefanywa na nguli hao, itazinduliwa rasmi siku hiyo na itakuwa maalum kwa watu kusikiliza nyimbo zake kisha Wanamuziki wate walioshiriki watapata fursa ya kuimba.

 

“Atakayekuja atajifunza mengi kutoka kwa Wanamuziki wakongwe mama, Zahir Ally Zorro, Nyoshi El Sadadt, Juma Kakere, Hassan Bitchuka na wengine wengi,” alisema Mbizo.

Leave A Reply