The House of Favourite Newspapers

Pigo Kubwa Brazil: Neymar Nje Mechi Mbili, Hofu Yatanda Kambini

0
Neymar kukosa michezo miwili ya Brazil kutokana na majeraha ya kifundo cha mguu

NEYMAR hatashiriki mechi mbili zijazo za Brazil za Kombe la Dunia baada ya kupata jeraha la mguu wa kulia, anasema daktari wa timu yao.

 

Mshambuliaji huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 30 aliondolewa uwanjani dakika ya 80 ya mchezo wa siku ya Alhamisi ambapo Brazil waliichapa Serbia 2-0 baada ya kukabiliwa vikali na Nikola Milenkovic.

Neymar Da Silva Junior

Neymar aliketi huku uso wake ukiwa umefunikwa wakati alipokuwa akipata matibabu na picha zilionyesha fundo lake la mguu wa kulia likiwa limevimba. Alielezea jeraha lake kama “moja ya nyakati ngumu zaidi katika kazi yangu”.

 

“Nimejeruhiwa, ndio sio vizuri, itaniumiza lakini nina uhakika nitakuwa na fursa ya kurejea tena kwasababu nitafanya kila liwezekanalo kuisaidia nchi yangu, timu yangu na mimi mwenyewe.”

Leave A Reply