The House of Favourite Newspapers

Sekondari ya John The Baptist Yafanya Mahafali ya 15 ya Kidato cha Nne 2022

0
Baadhi ya wanafunzi kwenye mahafali hayo.

 

SEKONDARI ya wasichana, John The Baptist iliyopo jijini Dar es Salaam, imefanya mahafali ya kumi na tano ya wanafunzi wanaomaliza kidato cha nne.

 

Akizungumza kwenye mahafali hayo yaliyofanyika Novemba 26 mwaka huu, Shuleni hapo, Mkurugenzi wa shule hiyo Daisy Mayanja amesema kuwa wanaishuru Serikali kwa kuendelea kuwa na shule binafsi ikiwa lengo ni kutoa elimu bora kwa wanafunzi nchini.

Mgeni rasmi Safu Majamba akikata utepe kuashiria mahafali hayo.

 

“Naishukuru serikali kwa kuwa bega kwa bega na shule za binafsi hii ni katika kuona tunapambana ili kutoa elimu bora zaidi na ndio maana sisi tunaajiri walimu wenye uweledi wa kutosha na taaluma ya kiwango cha juu ili tupate wanafunzi bora zaidi wenye ufaulu mkubwa katika masomo na stadi za kazi ambazo zitamuwezesha mwanafunzi kuwa na ujuzi wa kufanya hata kazi ya kujiajiri pindi atakapomaliza masomo yake.

 

“Hivyo basi tunawaasa wazazi na walezi kuwaleta watoto wao katika shule yetu ili waweze kupata elimu bora zaidi ambayo itawasaidia katika kupambana na soko la ajira,”amesema.

Nae Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Damiana Sagara, amesema kuwa amewashukuru wote kwa kuhudhuria katika mahafali hayo na ameahidi kufanya vizuri zaidi kitaaluma ili kuboresha nidhamu na taaluma shuleni hapo.

 

“Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutufikisha siku hii muhimu na pia namshukuru mkurugenzi wetu, Daisy Mayanja  ambaye ndio mwenye shule hii  kwa kuwekeza rasilimali zake  katika sekta ya elimu ambayo ndio msingi wa maendeleo ya nchi yetu.

 

“Shule yetu imekuwa ikipiga hatua mwaka hadi mwaka kitaaluma ikiwa viwango vya ufaulu kwa wanafunzi wa kidato cha nne ikiwa na masomo ya ujasiriamali yanayofundishwa katika shule hii.

 

“Shule inafundisha masomo ya ujasiriamali kama vile ushonaji na kazi mbalimbali za mikono ambazo zitamfanya mwanafunzi kujiajiri baada ya kuhitimu masomo.”

 

“Naomba nichukue fursa hii kuelezea kwa kifupi kuhusu maendeleo ya shule na changamoto zilizopo.

“Ndugu mgeni rasmi, shule hii ya John Baptist ni moja ya shule zilizopo ndani ya kata ya Bunju yenye usajili no S0283;

 

Ndugu mgeni rasmi, shule hii ya sekondari John The Baptist ilianza rasmi mwaka 2007, ikiwa na wanafunzi wachache na sasa hivi wameongezeka. “Shule ina vyumba vya madarasa na majengo ya kutosha na thamani zake kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita, ina waalimu wakutosha kama ilivyoelekezwa hapo awali na wenye uzoefu wakufundisha masomo mbalimbali yanayofundishwa katika elimu ya sekondari kidato cha kwanza hadi kidato cha sita.

 

“Hata hivyo shule ina walimu wa ziada kutoka Cannosa na Feza ambao wanafundisha muda wa ziada. Kutokana na ubunifu na uzoefu wa walimu wetu, wanafunzi wetu walikuwa wakifanya vizuri katika mitihani mbalimbali ikiwemo ya ndani na nje ya shule kulingana na uwezo wa kila mwanafunzi.

 

“Ili kuzidi kuweka walimu wetu katika ubora unaotakiwa wakati wote tumekuwa na ukaguzi wa ndani wa mara kwa mara pamoja na mafunzo ya sisi kwa sisi ili kuendana na mahitaji ya kitaaluma.

 

“Ndugu mgeni rasmi, uongozi wa shule pamoja na walimu tunayo mikakati ya kumuandaa mwanafunzi kujiandaa na mitihani na kuwa na utulivu. “Mlete mwanao John The Baptist apate elimu isiyo na shaka ndani yake”. Alimaliza kusema.

 

Pia mkuu huyo amewaasa wahitimu kwenda kuwasaidia wazazi mambo mazuri waliyofundishwa ikiwemo kushona na upishi pamoja na kazi za nyumbani.

 

Nae mgeni rasmi, Safu Majamba ambaye ni Meneja Msaidizi kutoka Kampuni ya Partner Coornestone Partiners Ltd amesema kuwa dhamira ya serikali ni kuona elimu inatolewa kwa kiwango cha juu na kila muhitimu kupata elimu na umahiri kumudu ushindani wa ndani na nje ya Nchi katika ajira na maendeleo ya jamii.

 

“Naipongeza shule kwa kutoa elimu kwa watoto wa kike pamoja na kwamba changamoto haziwezi kukosekana hivyo basi wazazi mna jukumu la kuijenga shule na mnahamasishwa kuleta wadogo zao hawa wahitimu waje wapate elimu bora kama hawa  na pia hata hawa wahitimu waje waendelee naasomo ya kidato cha tano hapa hapa.” Alimaliza kusema.

Leave A Reply