The House of Favourite Newspapers

Balama Apewa Program Maalum Morocco

0

LICHA ya kuwepo kambini nchini Morocco, lakini kiungo mshambuliaji wa Yanga, Balama Mapinduzi, ataendelea kufanya mazoezi binafsi kwa ajili ya kujiweka fiti.


Kiungo huyo yupo nje
ya uwanja kwa muda wa mwaka mzima akiuguza majeraha ya mfupa wa kifundo cha mguu aliyoyapata msimu wa 2019/2020.

 

Akizungumza na Spot Xtra, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela, alisema Balama atakuwepo sehemu ya kikosi hicho kwa msimu ujao baada ya kupona majeraha yake hayo.

 

Mwakalebela alisema kuwa, kiungo huyo hivi sasa yupo katika program maalum ya mazoezi kambini huko Morocco chini ya uangalizi wa madaktari wa timu hiyo.

 

“Balama amepona majeraha yake ya enka yaliyomuweka nje ya uwanja kwa muda mrefu, hiyo ndiyo sababu ya kumjumuisha katika msafara wetu wa Morocco ambako tumeweka kambi.

 

“Atakuwa sehemu ya kikosi chetu tutakachokitumia msimu ujao baada ya kupona na ili acheze anatakiwa kupona kwa asilimia mia moja, hivyo ataendelea na program hiyo kwa kipindi chote tutakachokuwepo hapa kambini Morocco huku akisubiri majibu ya madaktari,” alisema Mwakalebela.

WILBERT MOLANDI, Dar

Leave A Reply