The House of Favourite Newspapers

 Balozi Falme za Kiarabu ajitolea kusomesha watoto wa kike

Mkuu wa mkoa Dar es Salaam Paul Makonda akipokea hundi ya Shilingi milioni 20  kutoka kwa Balozi wa Falme za Kiarabu na wamiliki wa Erminet, Khalifa Abdul Rahman Al-Marzooqi (wa pili kulia),  ambazo zitatumika kama sehemu ya kuwasaidia wasichana waliofaulu masomo ya sayansi kwenye mitihani ya kidato  cha nne waweze kusoma kidato cha tano na sita.

BALOZI wa Falme za Kiarabu nchini na wamiliki wa Erminet, Khalifa Abdul Rahman Al-Marzooqi, wamejitolea kuwasomesha wanafunzi wa kike 100 wa shule na mkoa wowote ili kuchangia elimu kwa wanafunzi ambao wamefaulu masomo ya sayansi na kushindwa kuendelea na masomo hayo kutokana na changamoto ya kukosa ada.

Akizungumza katika hafla iliyotayarishwa na Makonda, Abdul Rahman alisema kuwa anamshukuru Makonda kwa kazi anazofanya katika kuhudumia jamii na kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na nchi yake.

 

Makonda na Balozi Al-Marzooqi wakipongezana. 

“Namshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kazi kubwa ambayo anaifanya ili kuleta maendeleo na kuimarisha ushirikiano  kati ya nchi zetu na tutaendelea kutoa ushirikiano katika maendeleo.

“Hivyo najitolea kuwasomesha watoto wa kike mia moja kwa mkoa wowote ambao wamefanya vizuri katika masomo ya sayansi na kushindwa kuendelea na masomo kutokana na kukosa ada,” alisema balozi huyo huku akishangiliwa.

 


Aidha Makonda amewataka madiwani wa wilaya kuchagua wanafunzi ishirini waliofauli masomo ya sayansi ambao hawana uwezo ili wapewe fedha hizo waweze kuendelea na masomo.

“Wanafunzi hao wawe na wazazi na hata wasio na wazazi,  kama hana uwezo wa kuendelea na masomo apewe fedha hizo,” alimalizia Makonda kwa kusisitiza.

Stori:Neema Adrian | GPL

Comments are closed.