The House of Favourite Newspapers

Tujitokeze kwa wingi kuiunga mkono Serengeti

TIMU yetu ya vijana Serengeti Boys leo inaingia uwanjani kuvaana na Uganda kwenye mchezo muhimu sana wa Kombe la Mataifa Afrika kwa Vijana. Huu ni mchezo muhimu kwa vijana wetu kwa kuwa walishapoteza mchezo wa
wamebakiza michezo miwili tu.

 

Wakishamalizana na Uganda watakuwa wanasubiri mchezo wa mwisho dhidi ya Angola na hivyo ni lazima washinde huu na huo unaofuata kama kweli wanataka kufuzu.

 

Serengeti hawawezi kufuzu kwa kwanza dhidi ya Nigeria na hivyo ili wapate nafasi ya kushiriki Kombe la Dunia kwa vijana wanatakiwa kushinda mchezo huu.

 

Vijana hao wanatakiwa kukusanya pointi sita ili kuwa na uhakika wa kufuzu kwa michuano hiyo kwa sasa wakiwa
nguvu zao wenyewe bali umoja na mshikamano wa Watanzania wote.

 

Nafikiri tunatakiwa kujitokeza kwa wingi uwanjani kuwaunga mkono kwa kuwa nguvu yetu inaweza kuwapa morali ya juu sana na kuwapa ushindi vijana wetu.

 

Tulipambana kwenye michezo ya Simba ya kimataifa, tukapambana kwenye michezo ya Taifa Stars na kuipa nafasi ya kwenda Kombe la Mataifa Afrika Championi tunafikiri leo ni siku yetu tena ya kuweka historia kwenye Uwanja wa Taifa na kuhakikisha tunakwenda kuwaunga mkono vijana hao ili tuweze kupata ushindi.

Comments are closed.