The House of Favourite Newspapers

Balozi Kombo Ampongeza Amitin Kurudisha Ngumi Zanzibar

0

Kwa mara ya kwanza, Balozi wa Tanzania nchini Italia, Mahmoud Thabit Kombo, amekutana na kuzungumza na Mratibu wa Tosh Sports Promotion, Amitin Mbamba, Wakiwa nchini Italia kwenye Wiki ya Kongamano la Uwekezaji na Biashara nchini humo ambalo kilele chake Kitafanyika Oktoba 19, 2023.

Balozi Kombo amempongeza Bi Amitin ambaye kampuni yake ya Tosh Sports Promotion imeufufua mchezo wa ngumi Zanzibar Baada ya Miaka 60 kupitia pambano lao lililofanyika mwezi Agosti visiwani humo.

Sambamba na hilo wamezungumza namna ya kuzitumia fursa na kushirikiana kwenye kuendeleza kukuza ngumi za kulipwa nchini.

Aidha Balozi Kombo ametoa wito kwa Watanzania kuchangamkia fursa zinazopatikana kupitia kongamano hilo ambalo ameliandaa kwa miaka mitatu mfululizo huku mwaka huu Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitarajiwa kuwa mgeni rasmi.

Leave A Reply