The House of Favourite Newspapers

Balozi wa Canada – Tanzania Ampongeza Diwani wa Kijichi

Diwani wa Kata ya Kijichi Bwana Elias Kassim Mtalawanje amekutana na kufanya Mazungumzo na Balozi wa Canada nchini Tanzania Bi.Pamela O’Donnell Ofisini kwake Mtaa wa Milambo Street Posta Jijini Dar es Salaam.

 

Diwani huyo akizungumza na Balozi wa Canada amesema Tanzania ni nchini yenye Vijana wengi ambao wamekuwa wakianzisha miradi midogo midogo huku wakihitaji msaada kidogo tu ili waweze kujikwamua na umasikini pamoja na kufikia ndoto zao.

Aidha Diwani huyo amemuomba Balozi wa Canada nchini Tanzania Bi. Pamela (Pichani) kuwasaidia kupata Visa vijana na wanafunzi wa vyuo vikuu nchini Tanzania ambao wanataka kwenda kusoma Elimu ya juu nchini Canada akisisitiza kuwa pindi watakapopata Ujuzi na Elimu wataweza kuja kuwasaidi vijana wenzao na Jamiii nzima ya Watanzania.

Balozi Pamela amempongeza Diwani huyo kwa namna anavyofanya kazi kwa bidii katika Kata yake na kusema Tanzania inapaswa kujivunia kuwa na Viongozi vijana kama yeye.

Amemwambia Diwani Mtalawanje asisite kumuona tena iwapo atakuwa anajambo anahitaji msaada wake na akamuahidi kuhudhuria kwenye project yake atakayoianzisha hivi karibuni.

 

Pia ameongeza kuwa amekuwa akimfuatilia Diwani Mtarawanje kupitia mtandao wa Twitter na kuvutiwa na namna amavyofanya kazi yake katika kata yake.

Comments are closed.