The House of Favourite Newspapers

BANDO YA AIRTEL MITANDAO YOTE YAZINDULIWA

Duka la Airtel  Money la Wilayani Babati Mkoani Manyara maalum kwa wateja na wakazi wa eneo hilo kurahisisha kupata huduma mbalimbali. 

Mkuu wa wilaya ya Babati Mkoani Manyara, Raymond Mushi akikata utepe kuzindua duka la Airtel ‘Airtel Money Branch’. Kushoto ni Meneja wa Airtel Mkoa wa Manyara, Polas Emmanuel.
Mkuu wa Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, Raymond Mushi, akizungumza jambo.
Baadhi ya wakazi wa eneo hilo wakishuhudia uzinduzi huo.

 

Mkuu wa wilaya ya Karatu Mkoani Arusha, Theresia Mahonga amewataka wakazi wa wilaya hiyo kutumia fursa ya uwepo wa mitandao ya simu za mkononi  kupashana habari za maendeleo na kufanya biashara salama kupitia huduma za fedha za mitandao hiyo, badala ya kuhamasishana katika vitendo vya kihalifu.

 

Mahongo amesema hayo wakati wa uzinduzi wa duka la Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel  katika wilaya hiyo, ambaye amesema kumekuwepo na tatizo la matumizi mabaya ya simu za mkononi jambo linalopaswa kukemewa ili mitandao hiyo iweze kuchangia maendeleo.

 Kwa Upande wa Babati, Mkuu wa wilaya ya Babati Mkoani Manyara, Raymond Mushi  amewataka wakazi wa wilaya hiyo, kutumia fursa za mitandao ya simu kutunza fedha zao wanazopata baada ya kuuza mazao yao kwani itawasaidia kurahisisha biashara zao pamoja na kuepuka uwezekano wa kuporwa fedha za mauzo.

 

“Wakulima wengi wanatoka katika maeneo ya Vijijini hivyo wanashindwa kuhifadhi fedha zao sehemu salama lakini iwapo wakitumia vyema duka hili watawaweza kutunza fedha kwa urahisi na kufikia malengo waliyokusudia,” alisema.

Meneja wa Airtel Mkoa wa Manyara, Polas Emmanuel (kushoto) akizungumza jambo.

 

Pia amesema zipo faida nyingi ambazo zimekuwa zikijitokeza kupitia huduma za kampuni ya simu za mikononi ya Airtel kwakusaidi jamii hususani katika suala la mawasiliano nafuu pamoja na kusaidia elimu nchini.

 

Meneja wa Airtel Mkoa wa Manyara, Polas Emmanuel, amesema kufunguliwa kwa duka hilo kunaenda sambamba na uzinduzi wa huduma ya Bando ya Airtel Mitandao yote ikiwa  ni utekelezaji wa mpango wa kampuni hiyo kutoa hudua nafuu na kusogeza huduma kwa jamii nchi nzima.

 

Naye msimamizi wa duka hilo, Jublet Mnyenye amesema duka litawawezesha vijana kupata fursa za kujiajiri kupitia huduma zinazotolewa na kampuni hiyo.

 

Amesema licha ya vijana kupata fursa za ajira lakini pia itawasaidia kuwa wabunifu kwakupata elimu ya ujasiriamali kupitia mtandao kwani wataweza kubadilishana mawazo na vijana wenzao hao  kupiga hatua kibiashara.

 

Baadhi ya watuamiaji wa huduma za Airtel wamesema watapata urahisi katika shughuli zao ikiwemo mawasiliano ya simu na miamala ya kifedha yakuweka pamoja na kutuma.

Comments are closed.