Kartra

Bangi, Dawa za Kienyeji Zakutwa Gerezani

Ukaguzi ambao ulifanyika alfajiri katika gereza la mji wa Empangeni ambalo liko Jimbo la Kwa-Zulu Natal nchini Afrika Kusini umebaini bangi zenye thamani ya dola 600, televisheni ya taifa ya SABC imeripoti.

 

Anayekaimu nafasi ya kamishina wa kitaifa wa gereza hilo bwana Makgothi Thobakgale ndio aliongoza ukaguzi huo katika kituo cha kurekebisha tabia cha Qalakabusha.

Gereza hilo limewahi kuvunjwa mara kadhaa katika miaka ya hivi karibuni , mwandishi aliongeza. Wafungwa wanne ambao walitoroka hivi karibuni. Zaidi ya simu za mkononi 30 na dawa za kienyeji ziliweza kupatikana wakati wa ukaguzi huo wa kushtukiza.


Toa comment