The House of Favourite Newspapers

Barabara ya NYERERE katika Makutano ya Shaurimoyo na Nyerere Kufungwa leo

0

Barabara ya NYERERE katika makutano ya Shaurimoyo na Nyerere inatarajiwa kufungwa leo kwa ajili ya ujenzi wa daraja la reli ya Kisasa ya SGR.

Kupitia taarifa yake kwa umma, Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Dar es Salaam inasema kuwa barabara hiyo itafungwa kuanzia kesho Jumapili Mei 28 hadi Jumamosi Septemba 30, 2023 baada ya ujenzi husika kukamilika.

Taarifa hiyo imesema katika kipindi hicho cha ujenzi, vyombo vyote vya moto pamoja na watembea kwa miguu wanashauriwa kutumia barabara ya Kawawa, Veta- Chang’ombe, Shaurimoyo, Kilwa Road na barabara ya mchepuko iliyojengwa pembezoni mwa eneo hilo la ujenzi.

TUKIO la KIGWANGALLA KUDAIWA KUMPIGA RISASI MLINZI WAKE, JESHI la POLISI LATOA UFAFANUZI…

Leave A Reply