The House of Favourite Newspapers

Kijana Ajirusha Kwenye Bwawa, Aliyemshuhudia Akizama Asimulia Tukio Zima – Video

0

Mtu mmoja aliefahamika kwa jina la Daud Lufungulo anayekadiliwa Kuwa na umri wa miaka 30 Mkazi wa mtaa wa Samina halmashauri ya Mji wa Geita Mkoani Geita amefariki dunia baada ya kujirusha kwenye Bwawa la maji wakati ameenda kuoga.

Mashuhuda walioshudia tukio hilo wamesema wamekuwa na kawaida ya kuoga eneo hilo na marehemu alifika katika bwawa hilo na kuwakuta wakioga pamoja na kufua nguo zao ndipo akawaomba sabuni pamoja na dodoki ili nae aoge baada ya kumumpa alivua nguo zote nakujirusha ndani ya bwawa hilo na kuzama moja kwa moja kwani hakuonekana tena ndipo wakaanza juhudi za kumuokoa lakini haikuwezekana.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Mkaguzi wa Jeshi la zima Moto na uokoaji wilaya ya Geita INSP. Wambura Fidel amesema sababu za kifo hicho ni kutokana na bwawa hilo kuwa na kina kirefu pamoja na tope nyingi hiovyo marehemu alijirusha na kunasa kwenye tope hizo nakusababisha kifo chake.

Leave A Reply