The House of Favourite Newspapers

Barabara Ya Sinza Maalum Kero Kwa Wananchi

barabara-mbovu-sinza-3Taswira ya miundombinu hiyo.barabara-mbovu-sinza-1…maji ya mvua yakionekana kutuwana katika miundombinu hiyo.barabara-mbovu-sinza-2 …hali halisi.

BAADHI ya wananchi wa maeneo ya Mapambano jijini Dar, wamelalamikia watengenezaji wa barabara ya kuelekea Shule ya Msingi, Sinza Maalum (Kijitonyama) kutokana na ujenzi wake kuonekana kusuasua.

Akizungumza na mtandao huu mmoja kati ya wakazi hao, Ramadhan Iddi alilalamikia ujenzi huo ambao ulianza miezi michache iliyopita ambapo ujenzi huo unaonekana kwenda taratibu kama si kuendelea kabisa.

“Kwa mfano nyakati za mvua huwa tunapata tabu sana kupita barabara hii kutokana na miundombinu ya barabara kuwa mibovu,” alisema Iddi.

Naye Neema Amos mkazi wa maeneo hayo alieleza malalamiko yake:

“Jamani tunaomba serikali iangalie upya barabara hii na ikiwezekana kama kuna uzembe wa kucheleweshwa kumalizika, wahusika wawajibishwe na ujenzi ukamilike haraka.

“Mwezi uliopita nilikuwa mjamzito, ndugu zangu walipata shida kunipeleka hospitali kwani ilitubidi kuzunguka umbali mrefu ili kutokea Hospitali ya Palestina lakini kama barabara ingekuwa imetengenezwa ingerahisisha,” alisema Neema.

Ili kupata majibu ya walalamikiwa, mtandao huu ulimtafuta mkandarasi wa barabara hiyo Eng. Godson Tenga na kumsomea malalamiko hayo ambapo alikuwa na haya ya kusema:

“Nakuomba ndugu mwandishi uende Halmashauri ya Kinondoni kwani wao ndio watakupatia majibu juu ya suala hilo mimi siwezi kulizungumzia,” alisema.

Na Denis Mtima/Gpl.

Comments are closed.