The House of Favourite Newspapers

Makamuzi Ya Twanga Ndani Ya Toroka Uje

twanga-pepeta2

Mwanamuziki mkongwe wa bendi hiyo, Luiza Nyoni akiendelea kufanya mavituz jukwaani kama alivyonaswa.

twanga-pepeta1Wanenguaji Otilia Boniface (kulia) na Maria Soloma wakiwajibika.

twanga-pepeta3

Mpiga gitaa la besi, Hosea Mgoachi akicharaza nyuzi kwa hisia.

twanga-pepeta4Sehemu ya mashabiki walioshindwa kuvumilia na kuvamia jukwaa.

twanga-pepeta5Sebene limechanganya, wanenguaji kazini.

twanga-pepeta7Rapa wa Twanga, Khalid Chokoraa akiweka vionjo vyake baada ya wimbo ‘Aminatha’ kuchanganya.

Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ Kisima cha Burudani, usiku wa kuamkia leo imefanya makamuzi ya nguvu kwenye Ukumbi wa Toroka Uje, uliopo Tabata Jijini Dar, ikiwa ni maazimisho ya kumbukumbu ya Hayati Baba wa Taifa, Hayati Julius Nyerere ‘Nyerere Day’.

Kama kawaida kundi zima la bendi hiyo likiongozwa na Ally Choki ‘Mzee wa Farasi’ liliwanogesha mashabiki na kuwafanya kuvamia steji na kujiachia kimadaha.

Bendi hiyo imeufanya ukumbi huo kuwa ukumbi wake wa nyumbani ambapo ‘itakongoli’ kila Ijumaa.

Comments are closed.