The House of Favourite Newspapers

Baraka Akiri Kutokuwa Sawa Na Naj

0

Baada ya tetesi kusambaa mitandaoni kuwa penzi la msanii wa Bongo Fleva Baraka Andrew ‘Baraka the Prince’ na Najma Dattan ‘Naj’ kwa sasa linapumulia mashine hatimaye mwenyewe amefunguka kuwa ni kweli.

 

Akipiga stori mbili tatu na gazeti hili Baraka ambaye kwa sasa anatamba na ngoma yake ya Sawa alisema ni kweli yeye na mpenzi wake Naj hawapo vizuri.

Alisema sababu kubwa ni yeye ndio alimzingua hivyo wapo katika harakati za kukaa chini na kumaliza tofauti zao.“

 

Ni kweli mimi na Naj hatupo sawa, lakini hii haimaanishi kuwa tumeachana, hapana kuna mambo tu mimi kama mwanaume nilizingua, ila hayahusiani na kumsaliti wala nini, kwa hiyo muda si mrefu tutakaa chini na kuyamaliza kikubwa,” alisema Baraka.

STORI: MEMORISE RICHARD | GAZETI LA AMANI

Leave A Reply