The House of Favourite Newspapers

Gomes Aitaka Rekodi ya Kibabe Caf

0

KOCHA Mkuu wa Simba Mfaransa, Didier Gomes amesema kuwa amepanga kumaliza hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika bila ya kufungwa huku akitamba kuanza na AS Vita nyumbani na kwenda kumalizana dhidi ya Al Ahly nchini Misri.

 

Simba ina nafasi nzuri ya kumaliza katika nafasi ya kwanza katika kundi lao A, ambao hivi sasa inaongoza kwenye Kundi A, wakiwa na pointi 10 wakifuatiwa na Al Ahly 7, AS Vita 4 na Al Merrikh 1.

 

Timu hiyo inatarajiwa kucheza mchezo wake tano wa michuano hiyo dhidi ya AS Vita ya Kinshasa, DR Congo mnamo Aprili, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Gomes alisema kuwa michezo yote mwili waliyoibakisha ni muhimu kwao katika hatua hiyo ya makundi, hivyo ni lazima washinde ili waweke rekodi.

Gomes alisema kuwa, kikubwa katika kuelekea michezo hiyo anataka rekodi ya kumaliza kundi wakiwa wanaongoza kundi lao na nyingine ni kutopoteza mchezo wowote kati ya sita watakayoicheza.Aliongeza kuwa hilo linawezekana kwake kutokana na ubora wa kikosi chake ambacho kinaundwa na wachezaji bora, uwezo na uzoefu wa kucheza michuano hiyo mikubwa ya kimataifa wanayoshiriki.

 

“Ninafahamu michezo hii miwili tuliyoibakisha ni migumu, lakini hiyo haitufanyi kuogopa na badala yake kujipanga na kufanya maandalizi ya kikosi changu.

 

“Uzuri mimi na wachezaji wangu tunajua tumebakisha michezo muhimu ambayo tunatakiwa tushinde ili tutengeneza rekodi mbili na moja ni kumaliza katika nafasi ya kwanza katika kundi letu na nyingine ni kucheza bila ya kufungwa.“Wapinzani wetu wote wamepoteza, tumebaki sisi pekee hivyo sitaki kuona tukipoteza katika michezo hii miwili kwa kuanza tunaanza na AS Vita hapa nyumbani kabla ya kwenda Misri kurudiana na Al Ahly,” alisema Gomes.Simba katika michezo minne waliyocheza wamefanikiwa kushinda mitatu na sare moja.

 

GOMES ATAKA STAILI HII YA MABAO SIMBA

Aidha, Gomes amefunguka kwamba anataka kukiona kikosi hicho kikiendelea kucheza kwa soka la pasi nyingi kutokana na staili hiyo kumfurahisha.Mfaransa huyo amesema kwamba staili hiyo ya uchezaji ya soka la pasi nyingi ambayo amekuwa akiifanya ndani ya kikosi hicho imekuwa ni nzuri kwa kuwa inawafanya pia wapate mabao mengi kwa wapinzani wao.

 

“Tunacheza soka la kumiliki mpira kwa muda mrefu hasa kwenye mechi zetu za karibuni, kwa namna hiyo inatufanya tuwe na umakini kwa muda mrefu sana.“Lakini inatufanya tuwe na uhakika wa kutengeneza nafasi za kufunga nyingi na pia tunatakiwa kuifanya staili hii kuendelea katika kila mechi zetu ambazo zinakuja,” alimaliza Mfaransa huyo.

Leave A Reply