The House of Favourite Newspapers

Baraza la Madiwani Laukataa Mkoa Mpya wa Chato

0

Baraza Maalum la Madiwani Halmashauri ya Wilani Geita Mkoa wa Geita wamepinga wilaya mpya ya Busanda pamoja na hifadi ya Taidfa ya Kisiwa cha Rubondo kuchukuliwa na mkoa mpya wa Chato unaotarajiwa kuanzishwa hivi karibuni wakidai kuwa itasababisha wananchi kusafiri umbali wa kilomita 200 kwenda kutafuta huduma na na kusababisha mkoa wa Geita kukosa sifa kiutawala.

 

“Tunaenda kupata huduma hii Chato kilomita zaidi ya 200. Sasa, ni namna gani tunazidi kuwaongezea wananchi wetu mzigo wakati wakihitaji huduma. Mimi naona mapendekezo haya yaheshimiwe…” Bw. Salehe Juma, Diwani wa Kata ya Nyarugusu.

 

Kisiwa cha Rubondo wakiache katika mkoa wa Geita kwasababu mkoa mpya ambao unaenda kuundwa, mkoa wa Chato, ukiangalia Ngara kuna misitu.

 

Mkuu wa wilaya ya Geita Fadhili Juma amaesema amepeleka mapendekezo Serikalini ya kukataa mpango huo wa kuchukua maeneo ya wilaya hiyo kwenda Chato kwakuwa yatasababisha athari kwa wananchi.

 

“Maazimio ambayo natoka nayo hapa na muhtasari, topo ridhaa kuacha kisiwa cha Rubondo lakini hatutakubali. Bora mkoa usipatikane kuliko wilaya ya Busanda kuingia kwenye mkoa mpya. Tuliwapa sababu zote kwamba ukitoa wilaya ya Busanda kwenye mkoa wa Geita maana yake mkoa wa Geita unakosa sifa za kuwa mkoa…”

 

Leave A Reply