The House of Favourite Newspapers

Barnaba, Meja Kunta, Kontawa Kukamua Shoo ya Nguvu kwa Wanavyuo

0

Wasanii maarufu Bongo, Barnaba, Meja Kunta, Kontawa, Platform, Lony Bway, Lody Music na wengine kibao, wanatarajiwa kukamua shoo ya nguvu kwenye Tamasha la Power Up Your Life.

Tamasha hilo litafanyika kwenye vyuo vikuu mbalimbali nchini na kufikia kilele chake katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Mabibo Hostel.

Tamasha hilo limeandaliwa na App ya Muziki ya Boomplay kwa kushirikiana na Itel kwa lengo la kutoa burudani kwa wanavyuo sambamba na kutambulisha bidhaa mpya kutoka Itel ya simu za Itel P55.

Tamasha hilo linatarajiwa kuanza leo Jumatatu, Januari 29, 2024 hadi Jumamosi, Februari 3, 2024, kupitia vyuo vikuu viwili, Chuo Kikuu cha Dar es Salam (UDSM) na Chuo Kikuu cha Ardhi.

Akizungumzia ushirikiano huo, Natasha Stambuli, Meneja Mkuu wa Boomplay Tanzania alisema:

“Tunafurahi kushirikiana na itel kuleta teknolojia bora na uzoefu wa burudani ya muziki kwa jamii ya wanafunzi nchini Tanzania.

“Ushirikiano huu unaenda sambamba na juhudi zetu za kupanua wigo wa usikilizaji wa muziki usio na kifani kwenye kupitia App yetu kwa watumiaji wetu na jamii inayowazunguka.

Kwa upande wake, Sophia Almeida, Meneja Uhusiano wa Umma wa itel Tanzania, alisema:

“Itel inafurahia kushirikiana na Boomplay katika kuimarisha maisha ya wanafunzi kote Afrika. Dhamira yetu ya kutoa teknolojia ya gharama nafuu na ubunifu inaambatana kikamilifu na ujumbe wa Boomplay wa kutoa uzoefu wa burudani ya muziki.

“Pamoja, tunaleta muziki na mwanga wa teknolojia kwenye vyuo vikuu, na kuunda kumbukumbu isiyofutika ya burudani na uvumbuzi barani Afrika.”

Leave A Reply