The House of Favourite Newspapers

Barua Nzito: Uwoya, Dogo Janja Mmejimaliza

0
Msanii wa Bongo Muvi, Irene Uwoya na mwanamuziki wa Bongo Fleva, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’ wakivalishana pete za ndoa.

 

NIANZE kwa kumshukuru Mungu kwa kunipa kibali siku nyingine kuweza kukutana nawe msomaji, pia wewe msomaji wa Barua Nzito kwa maoni na ushauri wako ambao ni muhimu sana.

 

Wiki hii barua yangu ninaomba iwafikie wanandoa wenye ndoa ya utata, dada yangu ambaye ni msanii wa Bongo Muvi, Irene Uwoya na mdogo wangu mwanamuziki wa Bongo Fleva, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’.

Nina imani hata kama mko kwenye fungate barua hii itawafikia. Miluzi ni mingi sana mitaani kuhusu ndoa yenu, siyo kwamba hamuendani ila kwa mila na tamaduni za Kiafrika ni nadra sana kuona mwanaume anaoa mwanamke anayemzidi umri kama ninyi.

Usipitwe na Matukio, Install App Yako ya Kijanja na Namba Moja Tanzania ya Global Publishers

Android ===>Google Play

iOS ===>Apple Store

Hata kama wapo ila wengi wao huwa hawajioneshi. Mwanaume kumzidi umri mwanamke imezoeleka kama jambo la kawaida ndiyo maana Dogo Janja kukuoa Uwoya imezua utata. Siyo kwamba hamuwezi
kuoana lakini mashabiki wenu wameshachoka na kuzizoea kiki zenu ambazo mmekuwa mkizifanya mara kwa mara pindi mnapotaka kuachia kazi mpya.

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’.

Sina shaka na umri kwani mapenzi hayana umri, dini, kabila au kipato kama wahusika wenyewe mmeridhiana lakini wasiwasi wangu ni namna ambavyo ndoa hiyo ina mkanganyiko. Kama kweli mmeoana basi Mungu awasimamie katika ndoa yenu, lakini kama ni kiki itakuwa imewashusha sana hata kama athari zake hazitajitokeza kwa sasa lakini zitakuwepo tu.

 

Kama si kiki ni ndoa ya ukweli basi Janjaro atakuwa amemuolea mwanaume mwenzake, maana inawezekana kwa baadhi ya imani. Mkanganyiko ni hata kitendo cha mama mzazi wa Dogo Janja kushindwa kuhudhuria ndoa ya mwanaye na ukisikiliza sababu zake zinaonesha ni za kupangwa, kwamba mama wewe utasema hivi na vile. Hakuna kitu muhimu kwa kina mama kama
kuhudhuria ndoa ya watoto wao au kuwaona na kuwabeba wajukuu zao.

Lakini napata wasiwasi pale mama Janjaro anapodai kuwa ameshindwa kuhudhuria ndoa ya mwanaye kwa sababu alikuwa na mambo mengine, hii haiingii akilini. Hili tu la mama Janjaro linatosha kufanya uone kabisa kuwa kwenye ndoa hiyo kuna kiini macho ndani yake.

 

Inaingia akilini kweli kwamba hata wazazi wa Uwoya ambao wapo karibu kushindwa kuhudhuria ndoa ya mtoto wao? Ndiyo kusema hata wao walikuwa na majukumu mengine ya muhimu kuliko sherehe ya pili ya mtoto wao? Hivi mnadhani Watanzania mashabiki wenu hawajui kupembua pumba na mchele, mlichofanya ni sanaa.
Kwa sababu hata mazingira na namna ndoa yenu ilivyofungwa haiendani na misingi ya imani kwa sababu ya baadhi ya vitu kwa upande wa bibi na bwana harusi.

Kama kweli mmefunga ndoa niwatakie kila la heri katika maisha yenu mapya lakini kama ni kiki mtakuwa mmewakosea sana mashabiki wenu. Naiona imani waliyokuwa nayo kwenu inavyoyeyuka na kuiua sanaa yenu na hata tasnia nzima.

 

Kwani kila mtakachokuwa mnakifanya watu watajua ni sehemu ya kiki. Nasema
ni kiki kwa sababu Uwoya alizungumza zaidi ya mara mbili na mwandishi wetu na akakanusha kuwa yeye hajaolewa bali picha zinazosambaa ni filamu. Mnapoendelea kushikilia kuwa ni ndoa basi itakuwa ni ndoa ya kipekee kwa mtindo wa maharusi walivyooana.

Barua Nzito na Gabriel Ng’osha Maoni&Ushauri: 0620 744 592

Usipitwe na Matukio, Install App Yako ya Kijanja na Namba Moja Tanzania ya Global Publishers

Android ===>Google Play

iOS ===>Apple Store

Leave A Reply