The House of Favourite Newspapers

Basata Yawaita Wasanii Wajadili Maslahi ya Kazi Zao

0
Makamu Mwenyekiti wa Cha cha Wanamuziki, Mzee Yusuf kutoka Safina Modern Taarab akizungumza kwenye mkutano huo. Kulia ni Rais wa Shirikisho la Filamu nchini TAFF, Eliah Mjata.

 

 

 

Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) limewaita wasanii wote nchini wakiwemo Bongo muvi, wanamuziki wa dansi, taarab na sanaa nyinginezo kwa ajili ya kuwapa somo na kujadiliana masuala mbalimbali ya kuisongesha tasnia hiyo.

Katibu Mtendaji wa Basata, Matiko Mniko akizungumza kwenye mkutano huo. Kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Washereheshaji nchini, Cyncia Henjewelle.

 

 

 

Akizungumza na wanahabari kwenye Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Jijini Dar, Kaimu Katibu Mtendaji wa Basata, Matiko Mniko amewataka wasanii wote nchini kuhudhuria kwenye mkutano huo muhimu utakaofanyika ukumbini hapo Septemba 29 mwaka huu.

Mkutano ukiendelea.

 

 

Matiko amesema kwenye mkutano huo wasanii wataweza kujadiliana mambo mbalimbali kwa ajili ya maendeleo ya sanaa hapa nchini.

Wanahabari kazini.

 

 

Katika mkutano huo pia Rais wa Shirikisho la Filamu nchini, (TAFF) Eliah Mjata ametumia nafasi hiyo kuwaalika waigizaji wote wa filamu nchini ili wajadilini kwa pamoja mambo yanayohusu tasnia hiyo.

 

 

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wanamuziki nchini, Mzee Yusuf naye amewaambia wanamuziki wenzake kuwa wajitokeze kwenye mkutano huo ili kueleza changamoto zao ili zitatuliwe na kuacha kusemea pembeni.

 

 

Wanamuziki wenzangu naomba tujitokeze kwenye mkutano huo ili tujadili masuala yetu mbele ya serikali yetu na tuache mambo ya kupenda kusemea pembeni kama tulivyozoea kwa maana hilo halisaidii.

Leave A Reply