The House of Favourite Newspapers

BASATA Yawapunguzia Adhabu Wasanii Watatu, Whozu, Bilnass na Mbosso

0

Baraza la Sana la Taifa (BASATA) limewapunguzia adhabu wasanii watatu, Whozu, Bilnass na Mbosso waliokuwa wamefungiwa na kutozwa faini ambapo sasa watalipa faini kisha ndiyo waruhusiwe kuendelea na kazi zao za sanaa.

Kikao cha kusikiliza rufaa ya hao kimefikia uamuzi huo  Novemba 14, 2023 baada ya wasanii hao kukata rufaa ambapo wametakiwa kulipa faini ili waweze kuruhusiwa kufanya kazi za sanaa nchini kwa kufuata maadili ya Kitanzania.

Kikao hicho kimeongozwa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Damas Ndumbaro katika ofisi zilizopo Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam ambapo wameondolewa adhabu za kufungiwa.

Pia Whozu amepewa saa sita ili kutekeleza azimio la kushusha wimbo huo kwenye “digital platforms” zote kama makubaliano yanavyoelekeza.

Waziri Ndumbaro amewaasa wasanii hao na wengine nchini kutumia ubunifu kwa kufuata taratibu ulioainishwa katika mwongozo wa uzingatiaji maadili katika kazi za sanaa.

#EXCLUSIVE: NAIRA wa JUAKALI AKANA KUMJUA DULLA MAKABILA -“SIMJUI, DADA YAKE SIJAWAHI KUMUITA WIFI”

Leave A Reply