The House of Favourite Newspapers

Bashe Acharuka Kenya Kuzuia Mahindi

0

SERIKALI nchini imesema imesikitishwa na kilichofanywa na Kenya kuzuia mahindi ya Tanzania bila kuwapa taarifa rasmi na kwamba kilichofanyika sio kitu cha kiungwana.

 

Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amefika leo Machi 7, katika mpaka wa Tanzania na Kenya uliopo Namanga na kushuhudia malori yakiwa yamezuiliwa kuingia Kenya kwa kile kilichoelezwa kuwa mahindi ya Tanzania yana sumu.

 

“Kinachofanyika mpakani ni uhuni ambao hatuwezi kuu – entertain, magari yanazuiwa kuingia Kenya wakati hakuna taarifa rasmi tuliyopokea,” alisema Bashe.

 

Hata hivyo Bashe amewapa matumaini wafanyabiashara na wasafirishaji wa mahindi ambao magari yao yamezuiliwa na kuwahkikishia kuwa serikali itachukua hatua za haraka kuhusu suala hilo.

Leave A Reply