The House of Favourite Newspapers

Basi Jipya Yanga SC Kama Ulaya

0

ACHANA na basi jipya la Simba ambalo walilitambulisha hivi karibuni, wadhamini wa Yanga ambaoni Kampuni ya GSM, imejibu mapigo kwa kushusha basi la kisasa aina ya Scania Irizar i6 ambalo ni zaidi ya lile la Simba.Simba walitambulisha basi aina ya TATA Marcopolo ambalo tayari limeanza kutumika kwenye safari za timu hiyo kwenye mechi zao, wakati huo huo mabosi wa Yanga wameshusha ndinga mpya ambayo ubora wake ni wa viwango vya kimataifa.

 

Spoti Xtra linakuletea kwa undani ubora wa basi hilo jipya la Yanga kwenye maeneo tofautitofauti ikiwa mabosi wao klabu hiyo wamefanya kufuru ya aina yake.

 

INJINI YAKE USIPIME

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali, basi hilo lina injini ya kisasa ambayo ni Scania DC09 112 (360hp), ni injini ambayo ina uwezo mkubwa na ni rafiki kwa mazingira.Inatumia mfumo wa kisasa wa kudhibiti matumizi makubwa ya mafuta na ina uwezo wa kufanya kazi kwenye mazingira yoyote. Pia ina mfumo wa gia nane ambao ni wa kisasa unaompa uhuru dereva kubadili kirahisi bila ya kutumia nguvu kubwa.

VITI VYA KUTOSHA

Basi hili lina jumla ya viti 50 ambavyo ni vya kisasa na vimewekewa mfumo wa USB ambao utawawezesha watakaopanda kuchaji kifaa chake kama vile simu, tablet, headphones na Ipad. Viti hivi ni vya kisasa ambavyo vitamuwezesha mtu kusafiri umbali mrefu bila kuchoka.

 

ISHU YA USALAMA SIYO POA

Kuhusu usalama kwenye basi hili ni wa kiwango cha juu, kila kiti kimewekewa mkanda wa kisasa ambao utamuwezesha mchezaji kuwa salama endapo kuna hitilafu inaweza kujitokeza.Pia basi hili lina mfumo wa kisasa ambao utampa taarifa dereva endapo kuna tatizo lolote linaweza kuhatarisha usalama.KIYOYOZI BINAFSIUkiachana na usalama kuwa wa hali ya juu, basi hili lina mfumo wa kiyoyozi binafsi

ambao humuwezesha abiria kuchagua kama anataka kula upepo au la.

WAZEE WA MUZIKI KILA KITU FRESHI

Basi hili pia limewekewa mfumo wa kisasa wa muziki ambao utawapa burudani watumiaji kusikiliza muziki wakiwa safarini jambo ambalo pia kwa kiasi kikubwa linasaidia kuondoa uchovu na msongo wa mawazo.

 

CHOO, FRIJI NDANI

Hakuna masuala ya kuchimba dawa njiani bwana! Unaambiwa basi hili la Yanga lina choo cha kisasa ambacho kitawawezesha watumiaji kumaliza haja zao huku basi likiwa kwenye mwendo bila kupata usumbufu wowote wakiwa safarini. Pia basi hili lina friji ya kisasa ambayo ina uwezo mkubwa wa kupoza vinywaji kwa ajili ya matumizi wakiwa safarini.

BOSI YANGA ATIA NENO

Mjumbe wa Kudumu wa Heshima wa Yanga, Tobias Lingalangala, alifunguka kuhusu ujio wa ndinga hilo akisema. “Tunawashukuru wadhamini wetu, shukran Gharib Said Mohammed kwa kutuletea mchuma huu, kwa sasa unaelekea gereji kwa ajili ya kuwekwa stika za klabu. Baada ya kuwekewa stika chuma kitakuwa zaidi ya dhahabu na almasi.”

Stori na Hussein Msoleka na Leen Essau, Dar

Leave A Reply