The House of Favourite Newspapers

Basi La Timu Lapinduka Na Kuua Wanne

ajali-marekaniMwonekano wa basi baada ya kupata ajali likiwa bado eneo la tukio.

NORTH CAROLINA, MAREKANI.

Watu wanne wamefariki dunia baada ya basi lililobeba wachezaji kutoka shule ya Ramah Jucco Academy  kupata ajali na kusababisha vifo vya watu wanne papo hapo.

Timu hiyo ilikuwa ikisafiri kutoka South Carolina kwenda kucheza na timu ya chuo cha God’s Chosen kilichopo Fayetteville, North Carolina. Kabla ya kugonga daraja na kupinduka.

Katika ajali hiyo watu wanne wamefariki dunia na wengine 42 kujeruhiwa vibaya na kukimbizwa hospitali. Wengi wa majeruhi hao ni kutoka Chuo Cha Clinton.

 

Comments are closed.