The House of Favourite Newspapers

Basi lapasuka gurudumu, abiria zaidi ya 50 wanusurika kifo!

0
  AJALI 1 Basi la Bongo Records lenye namba za usajili T 200 CAC jana limepata ajali katika eneo la Ngesha katika Wilaya ya Magu mkoani Mwanza baada ya kupasuka gurudumu la upande wa kulia na kuacha njia, umbali aa mita 60 kutoka barabara kuu ya Mwanza-Musoma. Hata hivyo katika ajali hiyo abiria zaidi ya 50 walinusurika kufa. Basi hilo hufanya safari zake kati ya Mwanza -Musoma -Busekela mkoani Mara.

ABIRIA AJALI 4
AJALI 2Baadhi ya abiria wakitaharuki huku  abiria mwenzao akiwa amelazwa chini baada ya kupoteza fahamu muda mfupi baada ya ajali hiyo kutokea.
ABIRIA WALIONUSURIKA AJALI 3Baadhi ya abiria waliokuwa wakisafiri na basi hilo wakiwa hawaamini kilichotokea.
DEREVA WA AJALI 5Dereva wa basi hilo akielekea kwenye buti kukata nyaya za umeme baada ya basi hilo kuacha njia kutokana na kupasuka kwa gurudumu lake la kulia na kuacha njia umbali wa mita 60 kabla ya kugonga mti. Magurudumu yote ya mbele yaling’oka na abiria wote hawakuumia.
AJALI 6
Na Mashaka Baltazar, Magu – Mwanza

ABIRIA zaidi 40  waliokuwa wakisafiri kwa  basi la Bongo Records linalofanya safari zake kati ya Mwanza-Musoma-Busekela Majita mkoani Mara, wamenusurika kufa baada kupasuka kwa gurudumu la mbele upande wa kulia wa basi hilo na kuacha njia.
 
Ajali hiyo ilitokea jana Juni 30 majira ya saa 9:20 alasiri kwenye barabara kuu ya Mwanza-Musoma katika eneo la Ngashe wilayani Magukatika Mkoa wa Mwanza ikiwa ni dakika chache baada ya basi kupita kituo cha mabasi cha mjini Magu.
 
Wakizungumza na gazeti hili eneo la tukio baadhi ya abiria wa basi hilo lenye namba za usajili T 200 CAC walisema chanzo cha ajali hiyo ni kupasuka kwa gurudumu la mbele na kusababisha liache njia na kuingia porini umbali wa mita 60 kutoka barabara kuu.
 
Baada ya basi hilo lililokuwa likitokea katika Kijiji cha Busekela Majita kupitia Musoma mjini liliacha njia  na kujikita kwenye mfereji wa mto ambapo bodi lake liligota chini na kujiburuza kabla ya kugonga mti na kusimama huku mmoja wa abiria hao ambaye ni mwanamke (jina halikufahamika)  alipoteza fahamu.
 
“ Tukiwa safarini gari lilikuwa katika mwendo kasi ambapo nilipitiwa suingizi lakini tulipofika Magu nilizinduka huku safari ikiendelea.Ghafla nilishangaa gari kuhama njia na kuingia porini  umbali wa kama mita 50 hivi ligonga miti,”alisema Ryoba Maliche mkazi wa Bugarika Mwanza ambaye katika ajali hiyo alipoteza simu ya mkononi.
 
Mwingine ni Peter Marwa yeye alisema kuwa wakiwa safarini alisikia mlio wa kitu kukatikamuda mfupi baada ya kutoka Magu mjini lakini dereva aliendelea na safari na ndipo ghafla alisikia mlipuko wa kupasuka kwa gurudumu.
 
“ Gari likiwa kwenye mwendo mkali nilisikia kishindo cha mlipuko wa kitu lakini sikufahamu kuwa ni gurudumu la gari.Basi letu liliingia upande wa kushoto mwa barabara hadi liliposimama nikagundua tumepata ajali,” alisema Marwa.
 
Alieleza kuwa waliposhuka chini walikuta deef ya mbele imeng’oka na kurudi katikati ya uvungu wa bodi ya gari na wakati lianacha njia baadhi ya abiria hasa akina mama walikuwa wakilia wakihofia usalama wao na kupoteza maisha.
 
Gazeti hili lilishuhudia abiria wakiwa wamejikusanya eneo la ajali hiyo wasijue la kufanya huku baadhi wakilalamika kuwa hawana nauli ya kusafirisha kutoka eneo la ajali hadi jijini Mwanza ambapo hakukuwa na majeruhi eneo hilo mbali na mmoja aliyepoteza fahamu.
 
Hata hivyo dereva wa basi hilo jina halikufahamika hakuwa tayari kuzungumzia ajali hiyo badala yake  alitumia muda mwingi akiwasiliana kwa simu na mmliki wa basi hilo.
 
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi alipopigiwa simu yake ilipokelewa na mlinzi wake na kudai yuko Kwimba kwenye kikao na kuomba atafutwe baadaye.
Ajali hiyo ni ya pili kujtokea ndani ya simu mbili ambapo Juni 29, mwaka huu basi moja la Kampuni ya Super Sami lenye namba T 449 BCB lilikokuwa likitokea jijini Dar es Salaam liligonga jiwe majira ya saa 7:00 usiku na kupinduka wilayani Misungwi.
 
Katika ajali hiyo watu watano walipoteza maisha popo hapo huku wengine 13 wakijeruhiwa na kulazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Misungwi na Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando Mwanza kwa matibabu.
Picha zote na Mashaka Baltazar/GPL, Magu – Mwanza
 
Leave A Reply