The House of Favourite Newspapers

Bassirou Faye Ashinda Uchaguzi wa Rais Senegal wiki moja Baada ya Kutoka Gerezani

0
Mgombea wa Urais kutoka kambi ya upinzani nchini Senegal, Bassirou Diomaye Faye.

Mgombea wa Urais kutoka kambi ya upinzani nchini Senegal, Bassirou Diomaye Faye ameshinda uchaguzi wa rais nchini humo ikiwa ni wiki moja baada ya kutoka gerezani.

Bassirou Diomaye Faye amechaguliwa kuwa Rais mteule wa Senegal akiwa na umri mdogo wa miaka 44 ambaye ataapishwa kuwa Rais wa Taifa la Senegal.

Rais huyo ameweka historia ya kuwa Rais mwenye Umri mdogo zaidi barani Afrika.

Katika uchaguzi huo, maelfu ya Wasenegali walijitokeza katika maeneo mbalimbali nchini humo wakisubiri kwa utulivu kupiga kura zao.

Abdoulaye Sylla, rais wa Tume ya Uchaguzi amesema idadi kubwa ya watu walijitokeza kupiga kura katika uchaguzi huo.

Mgombea wa ushirika wa utawala nchini Senegal ambaye alikuwa mgombea mwenzake kwenye nafasi hiyo, Amadou Ba amempongeza mpinzani wake kutoka kambi ya upinzani, Bassirou Diomaye Faye kwa kushinda uchaguzi wa Rais.

Wachache walikuwa wamesikia kumhusu mwaka mmoja uliopita na sasa ni Rais kamili.

Kuinuka kwa njia ya ajabu kwa Bassirou Diomaye Faye kunafikia kipindi cha hali ya juu katika siasa za Senegal ambazo ziliwavutia watu wengi.

Miezi ya kukaa jela pamoja na mshirika na mwanasiasa mwenye ushawishi, Ousmane Sonko iliisha ghafla, wawili hao wakiachiliwa wiki moja kabla ya uchaguzi wa urais.

MAZITO! SIRI za PENZI la LUKAMBA – KUINGIZIWA MA-EX NDANI na PENDEZA – LULU AYAMWAGA YOTE..

Leave A Reply