The House of Favourite Newspapers

Zoezi la Ubomoaji wa nyumba Bonde la Msimbazi Kuanza Rasmi Aprili 12

0
Mhandisi Humphrey Kanyenye, Mratibu wa Miradi ya Ushirikiano na Benki ya Dunia TARURA

Zoezi la ubomoaji wa nyumba zilizofidiwa na Mradi wa Uendelezaji wa Bonde la Msimbazi linatarajiwa kuanza rasmi Aprili 12, 2024, na litawahusu waathirika 2,155 ambao tayari wamelipwa fidia.

Hayo yamesemwa Machi 25, 2024 na Mhandisi Humphrey Kanyenye, Mratibu wa Miradi ya Ushirikiano na Benki ya Dunia TARURA alipokuwa akiongea na waandishi wa habari katika ofisi za mradi zilizopo Millenium Tower Kijitonyama, Dar es Salaam.

Mhandisi Kanyenye alieleza kuwa kwa mujibu wa makubaliano ya utekelezaji wa zoezi hilo, waathirika wa mradi ambao wameshapokea malipo yao wanatakiwa kuhamisha mali zao na kupisha eneo la mradi ndani ya wiki sita (6) baada ya kupokea fedha hizo kwenye akaunti zao.

Alieleza pia kuwa walichelewa kuanza zoezi hilo kwa ajili ya kuwapa muda waathirika wa mradi kubomoa wenyewe kwa hiyari ili kuokoa baadhi ya mali zao.

Aidha alisema kuwa kati ya waathirika 2,329 waliopo kwenye orodha ya daftari la kwanza la ulipaji fidia, kufikia tarehe 21 Machi 2024, tayari waathirika 2,151 walikuwa wamelipwa kiasi cha shilingi bil. 52.6.

Leave A Reply