The House of Favourite Newspapers

Bayo Na Imbori -29

0

Ilikuwa vigumu Dickson kuamini kilichotokea lakini ukweli ni kwamba kupatikana kwa Imbori ni jambo lililomfurahisha sana, walikumbatiana kwa furaha, baada ya kuachiana walikaa sehemu tulivu Imbori akaelezea nini kilitokea kuanzia kutekwa kwake hadi alipokutana na mzee Ramson aliyemsaidia kurudi tena mikononi kwa Dickson.
TAMBAA NAYO…

KUTOKANA na uoga aliokuwa nao Imbori juu ya usalama wa maisha yake baada ya chakula cha jioni, wakati wa kwenda kulala hakukubali kabisa kuwa peke yake, alimtaka Dickson walale pamoja lakini kwa masharti ya kuchukua chumba chenye vitanda viwili (Double bed).

Suala hilo Dickson aliliunga mkono huku moyoni akipania kuikata kiu yake ya muda mrefu ya kufanya mapenzi na msichana huyo, alipanga kulitimiza hilo kwa kutumia mbinu zake zote za kiushawishi.

* * *
“Mungu wangu!” Ilisikika sauti nzito ya mwanaume.
“Nini bosi?” aliuliza sekretari wake.
“Njoo uone.”
“Kuna nini?”
“Soma hii habari.”

“Hee! Si ndiyo huyu unayemtafuta kila siku.”
“Ndiyo.”
“Marekani alifikaje?”
“Nashindwa kuelewa”
“Mh!”

Taarifa aliyoisoma Bayo kupitia Mtandao maarufu wa habari wa Gossip Cop ilimshangaza sana, lilikuwa ni tangazo lililokuwa linatafuta mtu wa kujitolea figo kwa malipo ya fedha nyingi ili kuokoa maisha ya msichana mrembo Imbori Rohyah.

Bayo aliitazama kwa makini sura ya msichana huyo akagundua ndiye Imbori aliyekuwa anamtafuta kwa udi na uvumba, alijiuliza alifikaje Marekani na nini kilimpata lakini hakupata jibu, bila kupoteza muda alichukua mawasiliano yaliyoambatanishwa na tangazo hilo ili awasiliane na wahusika.

“Hallow, ” ilisikika sauti upande wa pili kwenye simu ya Bayo.
“This is Bayo.” (Huyu ni Bayo)”
“I am listening.” (Nakusikia)
“I found an ad through Gossip Cop blog , I need to donate kidney” (Nimeona tangazo kupitia Mtandao wa Gossip Cop, nahitaji kujitolea Figo.)
“Sure?” (Kweli?)
“Yes.” (Ndiyo)

“Where are you?” (Uko wapi?)
“Tanzania?” (Tanzania)
“Ok, give me a time i will contact you.” (Sawa, nipe muda nitawasiliana na wewe.”
Baada ya kukata simu Bayo alishusha pumzi ndefu, alijiuliza huyo aliyewasiliana naye alikuwa ni nani na alikuwa na uhusiano wa namna gani na Imbori lakini hakupata jibu, aliamua kuwa mvumilivu huku upande fulani wa moyo wake matumaini ya kumpata mpenzi wake Imbori yakianza kufufuka.

Dakika zikazidi kusonga mbele, akiwa hana hili wala lile baada ya saa mbili kupita simu ya Bayo iliita alipopokea alikutana na sauti ya mtu aliyejitambulisha kwa jina la Kamugisha Rweyimamu, ofisa wa masuala ya usafiri wa anga Dar es Salaam aliyemwambia kuwepo tiketi kwa ajili yake ya kwenda nchini Marekani iliyogharamiwa mpaka maradhi.

Pia alimuuliza angependa kusafiri lini, Bayo alijibu ikiwezekana siku hiyohiyo, kila kitu kitakwenda kama alivyotaka, baada ya kufanya maandalizi ya haraka usiku wa siku hiyo Bayo alikuwa ndani ya ndege ya Shirika la Anga la Eastern Far akisafiri kuelekea nchini Marekani.

Akiwa kwenye siti alikuwa kimya mno, hata pale alipoongeleshwa na msichana mrembo Rebecca aliyekuwa amekaa kwenye siti pembeni yake hakuweza kusikia lolote, muda wote alikuwa akiwaza nini kingetokea baada ya kukutana na Imbori.

Safari ilizidi kupamba moto hatimaye baada ya saa ishirini na sita za safari Bayo alikuwa Marekani akapokelewa na Dickson aliyekwenda naye hadi nyumbani kwake.
“What’s up Mr. Bayo?” (Hali yako bwana Bayo?) Dr. Donard Mand, mtaalam wa upasuaji wa figo aliyeandaliwa na Dickson kwa ajili ya kazi hiyo alimuuliza Bayo.
“Cool.” (Nzuri.)

“Do you real wanna donate a kidney?” (Ni kweli uko tayari kuchangia figo?)
“That’s fool question!” (Hilo swali la kipuuzi!)
“We wanna be sure man.” (Tunataka kupata uhakika)
“Is why am here.” (Ndiyo maana niko hapa)

“Ok, then before you have to check effection in your kidney, blood group, antigens and finally crossmatching.” (Sawa, lakini kabla unatakiwa kupima maambukizi katika figo yako, grupu la damu, antijeni na mwisho uwezekano wa muingiliano wa kubadilishana figo.)

“No problem.” (Hakuna tatizo.)
Hivyo ndivyo hali ilivyokuwa, Bayo alikuwa tayari kufanya lolote lile ili kuyaokoa maisha ya msichana aliyempenda sana kuliko kitu chochote kile duniani, zaidi alikuwa amepania kumrudisha tena kwenye mikono yake.

Asubuhi ya siku iliyofuata Bayo aliongozana na Dickson pamoja na Dr. Mand hadi David Louis Hospital & Kidney alikokuwa amelazwa Imbori kwa ajili ya kumchukua Bayo vipimo ili kuhakikisha kama alikuwa na sifa za kutolewa figo moja ambayo ingemsaidia Imbori aliyekuwa katika hali mbaya kwa wakati huo.

Je, nini kitaendelea? Tatizo nini hadi Imbori atakiwe kubadilishwa figo? Usikose wiki ijayo.

Leave A Reply