The House of Favourite Newspapers

Behind the scene ‘Saka Hela’ ya Nay wa Mitego ilivyonoga Sauz

0

Nay (1) Nay (2) Nay (3) Nay (4) Nay (5) Nay (6) Nay (7) Nay (8) Nay (9) Nay (10) Nay (11) Nay (12)

BONIFACE NGUMIJE

WIKI hii lokesheni tuko na kichupa cha mkali wa michano Bongo, Emmanuel Elibariki ‘Nay Wa Mitego’ kiitwacho Saka Hela.

Audio ya Saka Hela imefanyikia pale Free Nation kwa Mr. T-Touch na kichupa kimegongwa Sauz na dairekta mtasha aitwaye Nick ambaye pia ndiye aliyegonga kichupa cha Harmonize cha Wimbo wa Bado.

Kwa mujibu wa Nay wa Mitego kichupa hiki kimegharimu takribani shilingi milioni 40 za Kibongo. Wamekaa lokesheni kwa muda wa siku zisizopungua tatu na Video Queens waliohusika ndani ya kichupa hicho ni zaidi ya 20 huku magari ya kifahari kadhaa yakikinogesha.

“Kichupa ni kikali na kiukweli kimezidi kuniongezea fun base kutoka sehemu tofautitofauti Afrika, nafikiri ni hatua nzuri kwangu na Mungu akipenda sitarudi nyuma, ni mwendo wa kimataifa zaidi,” alisema Nay.

Sasa nakuchukua wewe msomaji kisha nakubwaga lokesheni, pwaah!Ona mapicha!

Leave A Reply