The House of Favourite Newspapers

Bei Za Mafuta Zapanda, Kuanza Kutumika Leo Mei 1, 2024

0

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imetangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini zitakazotumika kuanzia Jumatano, tarehe Mei 1, 2024 saa 6:01 usiku.

Kwa mwezi Mei 2024, bei za rejareja katika Mkoa wa Dar es Salaam ni petroli Tsh 3,314, Dizeli Tsh 3,196 na mafuta ya taa Tsh 2,840, Mkoa wa Tanga petroli Tsh 3,360, Dizeli Tsh 3,242 na mafuta ya taa Tsh 2,886 wakati Mtwara petroli Tsh 3,317, Dizeli Tsh 3,200 na mafuta ya taa Tsh 2,913.

Bei za jumla katika Mkoa wa Dar es Salaam ni petroli Tsh 3,181.48, Dizeli Tsh 3,063.68 na mafuta ya taa Tsh 2,709.68, Mkoa wa Tanga petroli Tsh 3,184.05, Dizeli Tsh 3,069.46 wakati Mtwara petroli ni Tsh 3,185.05 na Dizeli Tsh 3,067.90.

Taarifa ya EWURA ye leo Mei 1, 2024 imebainisha kuwa mabadiliko ya bei za mafuta kwa mwezi Mei 2024 yamechangiwa na ongezeko la bei za mafuta yaliyosafishwa katika soko la dunia (FOB) kwa wastani wa asilimia 3.90 kwa mafuta ya petroli na kupungua kwa wastani wa asilimia 1.31 kwa mafuta ya dizeli;

Kupungua kwa gharama za uagizaji mafuta (premiums) kwa wastani wa asilimia 7.21 kwa petroli na kwa wastani wa asilimia 2.15 kwa dizeli kwa Bandari ya Dar es Salaam; wastani wa asilimia 10.14 kwa petroli na wastani wa asilimia 23.18 kwa dizeli kwa Bandari ya Tanga; na wastani wa asilimia 5.32 kwa mafuta ya petroli na dizeli kwa Bandari ya Mtwara.

Aidha, mabadiliko hayo yamechangiwa na kubadilika kwa kiwango cha kubadilishia fedha za kigeni (exchange rate) na kuendelea kutumia EURO kulipia mafuta yaliyoagizwa.

‘SWIPE’ KUSHOTO kuona taarifa ya Bei za mafuta za rejareja kwa maeneo mbalimbali ya miji, wilaya na mikoa.

 

Bei Za Mafuta Zapanda, Kuanza Kutumika Leo Aprili 3, 2024

Leave A Reply