Bei Za Mafuta Zapanda, Kuanza Kutumika Leo Aprili 3, 2024
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), imetangaza bei mpya za mafuta zitakazoanza kutumika leo Jumatano Aprili 3, 2024 huku bei ya Petroli na dizeli zikipanda ikilinganishwa na mwezi Feburuari.