The House of Favourite Newspapers

Beki La Kumwaga Maji Lapewa Ofa Nono, Lasaini Yanga

0
Joyce Lomalisa

MENEJIMENTI ya beki wa kushoto wa Yanga raia wa DR Congo, Joyce Lomalisa imefikia makubaliano mazuri ya kuongeza mkataba mwigine wa mwaka mmoja wa kuendelea kubakia hapo kwa msimu mwingine mmoja na nusu katika timu hiyo.

Lomalisa ambaye anasifika kwa kupiga krosi safi ‘kumwaga maji’, alibaza miezi sita katika mkataba wake ambao ulikuwa unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu.

Beki huyo amerejea uwanjani hivi karibuni katika Kombe la Mapinduzi akitokea katika majeraha ya enka aliyoyapata katika mchezo wa Makundi wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly ya nchini Misri.

Mmoja wa Mabosi wa Yanga kutoka ndani ya Kamati ya Mashindano ya timu hiyo, ameliambia Championi Jumatano kuwa, beki huyo ameongezewa mkataba wa mwaka mmoja wenye ofa kubwa uliomshawishi ‘kusinya’ tena.

Bosi huyo aliongeza kuwa, beki huyo amekubali kusaini baada ya kumboreshea baadhi ya mahitaji yake aliyoyahitaji, ikiwemo mshahara na dau la usajili alilohitaji kwa viongozi hao kabla ya kusaini mbele ya meneja wake anayemsimamia.

Aliongeza kuwa uwezo na uzoefu wa kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika na Ligi Kuu Bara, ndiyo umemshawishi Kocha Mkuu wa timu hiyo, Muargentina Miguel Gamondi kupendekeza kumbakiza Yanga.

“Jana (juzi) kabla ya dirisha kufungwa, viongozi wetu wa Yanga na meneja wa Lomaisa tulikutana na kumpa ofa yetu na yeye kutupa yake na kufanya mazungumzo ya kumuongezea mkataba mwingine.

“Makubaliano hayo yalifikia sehemu nzuri na kufikia makubaliano mazuri ya kumuongezea mkataba mnono ambao yeye mwenyewe mchezaji na meneja wake wameridhika na kusaini.

“Ni mkataba wa mwaka mmoja pekee aliousaini, hivyo atakuwa na mwaka mmoja na nusu wa kubakia Yanga, kwani alibakiza miezi sita,” alisea bosi huyo.

Rais wa Yanga Injinia Hersi Said juzi alizungumzia hilo kwa kusema kuwa: “Tunatengeneza timu itakayokuwa bora na tishio katika Ukanda huu wa Afrika, hivyo hatutamuchia mchezaji yeyote aliyokuwepo katika mipango ya kocha wetu.”

NOVATUS AIPONZA TAIFA STARS -WAPOKEA KIPIGO KIZITO /KISA MADENI WACHEZAJI WATIMKA SINGIDA FG

Leave A Reply