The House of Favourite Newspapers

Beki Yanga: Nitawaweka Mfukoni Okwi, Kichuya

0
Gadiel Michael.

SIKU chache tangu atue Yanga, beki mpya wa timu hiyo, Gadiel Michael amefunguka kuwa ata­hakikisha anawazima washam­buliaji wa Simba, Emmanuel Okwi na Shiza Kichuya wataka­pokutana wiki ijayo.

Simba na Yanga zinatarajiwa ku­kutana katika mchezo wa Ngao ya Jamii, Agosti 23, mwaka huu, am­bapo tayari presha imekuwa kubwa, Yanga wamefunga safari kutoka Dar es Salaam hadi Unguja kwa ajili ya kambi kujiandaa na mchezo huo.

 

Beki huyo wa kushoto amejiunga na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Azam FC ambapo juzi Jumamosi katika mchezo wa kirafiki uliopigwa kwenye Uwanja wa Chamazi dhidi ya Ruvu Shooting al­ionyesha uwezo mkubwa wa kukaba na kupandisha mashambulizi.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Gadiel alisema kuwa kwake mchezo huo utakuwa ni wa kawaida na amejipanga kuwadhibiti wachezaji hao watakaocheza kwe­nye eneo lake hadi kusahauliwa na mashabiki wa timu yao.

 

“Nadhani hiyo ndiyo mechi am­bayo nitajitambulisha rasmi Yanga maana katika kucheza kwangu mpira sijawahi kuogopa mechi kub­wa hata siku moja wala kuwahofia wachezaji, na hao ambao watakuwa wanafika kwenye eneo langu wajue kabisa nitawazima kabisa siku hiyo.

“Lakini hata wakati nacheza Azam, mechi za Simba na Yanga nilikuwa nikiaminiwa kupewa nafasi kwa sababu kuna kitu ninachokionyesha, sasa Yanga nahitaji kuaminika zaidi pia naamini Mungu ataniongoza kwa kila kitu katika maisha yangu mapya,” alisema Gadiel.

 

Katika siku za hivi karibuni, beki huyo amekuwa akionyesha uwezo wa juu hasa alipokuwa akiichezea timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, kiasi cha kuaminiwa na kuwa na uhakika katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo licha ya kuwa ni chipukizi.

Usajili wake kutua Yanga uliam­batana na ugumu baada ya awali Azam FC kugoma kumuachia kuto­kana na kuwa na mkataba ambao ulitarajiwa kumalizika Desemba, mwaka huu, lakini baada ya mazun­gumzo baina ya klabu hizo, akaachi­wa kwa ada ya uhamisho wa shilingi milioni 10.

 

Ibrahimu Mussa, Dar es Salaam

 

===

Usipitwe na Matukio, Download na Install ==> Global Publishers App

VIDEO: Haji manara; Tunaenda Zanzibar Tutawapiga Yanga

Leave A Reply