The House of Favourite Newspapers

Bella Aacha Kichanga, Aponda Raha Zenji!

UBUYU mtamu ukiumung’unya tu mdomoni unajitanabaisha wenyewe hasa ukiumung’unya ukiwa umepikwa Kipwanipwani, ndiyo unanoga zaidi!

Sasa ubuyu ukufikie kuwa, mwigizaji ambaye pia ni msanii wa Bongo Fleva, Isabela Mpanda ‘Bella’, anadaiwa kuacha kichanga cha miezi mitatu na kwenda kula bata visiwani Zanzibar au Zenji.

Kwa mujibu wa msambaza ubuyu wetu, hivi karibuni Bella alinaswa kwenye hoteli moja visiwani humo iliyojulikana kwa jina la Coral Beach akiwa na mlezi wa Bongo Muvi, Catherine Ambakyise ‘Mama Lola’ wakila bata la hatari.

SIKIA CHANZO

Chanzo ambacho ni rafiki wa karibu wa Bella kililimwagia ubuyu Ijumaa Wikienda kwamba, hata marafiki zake

wanamshangaa mno

shoga yao huyo kwa kitendo alichokifanya cha kumwacha

mtoto wake huyo mdogo na kwenda kula bata.

Kilidai kwamba, Bella amekuwa akiponda raha Zanzibar yapata wiki moja huku mwanaye huyo ikiwa haijulikani kama amemwachisha kunyonya au la!

“Mpaka sasa hivi mimi simwelewi kabisa Bella. Sijui ni nini kimempata maana ninavyomjua ni mama bora sana kwa watoto wake. Siamini kama anaweza kumuacha mtoto mdogo, tena wa umri wa miezi mitatu anayenyonya na kwenda kustarehe muda wote huo,” kilifunguka chanzo hicho.

IJUMAA WIKIENDA NA BELLA

Baada ya kuunyaka ubuyu huo, Ijumaa Wikienda lilimsaka Bella kwa njia ya simu yake ya kiganjani, lakini hakupatikana.

Kwa kuwa mnyetishaji alitonya kwamba Bella yupo na mama Loraa, Ijumaa Wikienda lilimwendea hewani mlezi huyo wa Bongo Muvi ambapo aliombwa msaada wa kuzungumza na Bella, akafanya hivyo.

Ijumaa Wikienda: Mambo vipi Bella? Nina shida na wewe, je, tunaweza kuzungumza?

Bella: Poa, mimi nipo Zanzibar,

labda nikirudi tutaongea.

Wikienda: Lakini mtoto wako mchanga umemuachia nani?

Bela: Kwani kuna tatizo gani? Au unajua amebaki na nani? Najua umepiga kwa ajili ya hilo, mimi sitaki kabisa mambo ya magazetini.

Wikienda: Sasa huko umeenda kikazi au?

Bela: Mimi naomba, sitaki kuzungumza hilo, wewe jua tu mwanangu yupo sehemu salama, hana shida yoyote na ninakuomba sana, sitaki habari hii itoke gazetini kwa sababu sijawahi kukunyima ushirikiano (akakata simu).

MSIKIE MAMA LORAA

Baada ya kuzungumza na Bella kisha akakata simu, Ijumaa Wikienda lilipiga kwa mara nyingine ili kuzungumza na mama Loraa ambapo aliulizwa kuhusu Bella kujiachia na kumwacha mwanaye mdogo.

Mama Loraa alifunguka kuwa, alikwenda Zanzibar na Bella kwa sababu maalum kwani tangu ajifungue alikuwa ndani hivyo alimpeleka kwa ajili ya kumpomgeza kwa kutoka kwenye uzazi usalama.

“Kwani kuna shida gani kumleta huku kupunga upepo? Sisi wote ni watu wazima hasa mimi ni mama, siwezi kumuacha mtoto kwenye sehemu ambayo siyo salama, itakuwa ngumu kufanya hivyo!”

Comments are closed.