The House of Favourite Newspapers

Ngoma Aenda Kuombewa kwa TB Joshua

IMEELEZWA kuwa, mshambuliaji mpya wa Azam FC, Donald Ngoma raia wa Zimbabwe, wikiendi iliyopita alienda kufanyiwa maombi maalum na mchungaji maarufu nchini Nigeria, Temitope Balogun Joshua ‘TB Joshua’

Katika maombi hayo ambayo yaliyofanyika kwenye kanisa la mchungaji huyo nchini Nigeria na kurushwa na runinga yake ijulikanayo kwa jina la Emmanuel TV, Ngoma alionekana akiombewa kwa kushikwa goti lake la mguu wa kulia ambalo limekuwa likimsumbua kwa muda mrefu.

Tatizo hilo la goti limemfanya Ngoma akae nje ya uwanja kwa muda mrefu na sasa anatarajiwa kurudi uwanjani mwezi ujao na kukosa baadhi ya mechi za mwanzo za msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

Ikumbukwe kuwa, Ngoma aliyejiunga na Azam hivi karibuni akitokea Yanga baada ya mkataba wake kuvunjwa kutokana na matatizo hayo ya goti, alipelekwa Afrika Kusini kufanyiwa matibabu ya kina na hivi karibuni anatarajiwa kurudi uwanjani.

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Comments are closed.