The House of Favourite Newspapers

Bella, Kibao Msambwanda Dar Live leo

0

BELLAKING of the Best Melodies, Christian Bella ‘Obama’ wakali wa kuyakata mauno Bongo, Kibao Msambwanda pamoja na mkali wa Singeli, Man Fongo a.k.a mzee wa Hainaga Ushemeji, leo (Septemba 3) wanatarajia kuangusha bonge la shoo ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar.

Akizungumza na BMM, mratibu wa shoo hiyo inayotambulika kama Usiku wa Nishike, Hartman Mbilinyi alisema kuwa, ile siku ambayo mashabiki wa burudani walikuwa wakiisubiri kwa hamu imefika na kwamba wajitokeze kwa wingi.

“Kwa kiingilio cha shilingi 10,000 tu, utapata kuimba na kucheza live na mkali Bella pamoja na Man Fongo bila kusahau kushuhudia na kucheza na Wana-kibao Msambwanda. Tukutane Dar Live tuweke historia ya pamoja,” alisema Hartman.

Leave A Reply