The House of Favourite Newspapers

Bella Kutoa taji kwa Pam D, Gigy Dar Live kesho

0

WAKATI mambo yakizidi kuwa moto kuelekea Mei 6 (kesho) katika mpambano wa kuimba kati ya Pamela Daffa ‘Pam D’ na Gift Stanford ‘Gigy Money’ ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo MbagalaZakhem jijini Dar, refa wao ambaye pia ni King of The Best Melodies, Christian Bella ‘Obama’ anatarajiwa kutoa taji kwa mshindi.

Akizungumza na Showbiz, Meneja na Mratibu wa Dar Live, Juma Mbizo alisema kuwa, shoo nzima ya kesho inatarajiwa kuanza saa mbili usiku ambapo Bella pamoja na bendi yake ya Malaika wataanza kwa kutoa burudani ya nguvu kwa kupiga nyimbo zao zote kali.

“Mashabiki wajipange na wajiandae kwa shoo ambayo tangu mwaka uanze Bella hajawahi kuifanya. Hiyo ni fursa kubwa mashabiki wote wanaoizunguka Dar Live na Dar es Salaam kwa ujumla. “Usiku huo zitapigwa nyimbo zote kuanzia Yako Wapi Mapenzi, Nashindwa, Nani Kama Mama, Msaliti, Nishike na nyingine kibao,” alisema Mbizo na kumalizia kuwa kiingilio kitakuwa shilingi 7,000 tu.

Naye Bella alitia neno kuwa kwa mara ya kwanza tangu aanze muziki atakuwa refa katika mpambano wa Gigy Money na Pam D ambapo bingwa atapata tiketi moja kwa moja ya kutengeneza naye kolabo na video. “Wote wanajulikana kama ni wasanii ambao ni wazuri. Kila mmoja ana jina hivyo ni wakati wa wewe shabiki kuamua nani mnaona anafaa nifanye naye kolabo.

Leave A Reply