The House of Favourite Newspapers

Ben Branko: Tatizo Siyo Filamu za Nje, Dawa ni Hii

0
Msanii maarufu katika tasnia ya uigizaji Bongo, Ahmed Abdul ‘Ben Branko’ au Serengo.

NA BRIGHTON MASALU | IJUMAA |MAKALA

WIKI hii tunaye msanii maarufu katika tasnia ya uigizaji Bongo, Ahmed Abdul ‘Ben Branko’ au Serengo.
Nimezungumza naye na kufunguka mambo kibao kuhusu fani yake hii iliyompa mafanikio makubwa katika
maisha yake. Fuatilia hapa chini…
IJUMAA:Ni lini haswaulianza kujihusisha na uigizaji?
BEN:Nilianza mwaka 1997nilipojiunga na Kaole Sanaa Group.
IJUMAA: Nani aligundua kama unaweza kuigiza kabla ya kujiunga na uigizaji?
BEN: Babu yangu (aliyemzaamama mzazi), marehemu Mzee Pwagu ndiye alinishawishi kujiingiza katika masuala ya uigizaji, akiamini kuwa nina kipaji na uwezo mzuri katika fani hiyo.
IJUMAA: Wakati unajiunga Kaole, ni wasanii gani uliwakuta?
BEN: Walikuwepo Swebe Santana, Jerry, Dk. Cheni, Mashaka, marehemu Mzee Kipara, marehemu babu (Pwagu) na wengine wengi.


IJUMAA: Wakati huo kundi lilikuwa likifanyia wapi kazi zao? Yaani tayari walikuwa wameshaanza kuonekana runingani?
BEN: Walikuwa na wiki kama moja hivi au mbili kama sikosei, wakiwa wanarusha igizo lao kwenye runinga ya ITV, mimi nilianza kuigiza igizo lililofuata liitwalo Hujafa Hujaumbika, baada ya kufanya mazoezi ya nguvu, niliigiza kama mtoto mhuni na mwizi.
IJUMAA: Baada ya hapo ikawaje?
BEN: Likafuata Igizo la Jahazi ambapo niliigiza kama mtoto wa tajiri nisiyependa kusoma, nikijivunia utajiri wa nyumbani, dada yangu aliikuwa Nora na baba yangu akiwa marehemu Mzee Bomba.
IJUMAA: Wakati huo nani alikuwa mwalimu wenu kundini?
BEN: Mwalimu wa mazoezi alikuwa Kahabi, baadaye akawa Julieth Samson ‘Kemmy’ kisha Chrisant Mhenga akachukua mpini.

Mzee Majuto.

IJUMAA: Wakati huo tayari sasa umeshaanza kuzoea uigizaji, siyo?
BEN: Kufi kia hapo nikaanza kutunga stori za maigizo ya uchekeshaji ya Mizengwe, achana na hii ya akina Mkwere, wakati huo alikuwepo marehemu Max.
IJUMAA: Maigizo mengine ni yapi yaliyofuata?
BEN: Ni mengi lakini ninayoyakumbuka ni pamoja na Zizimo, Tufani, Sayari, Taswira, Demokrasia, Gharika kabla ya kumaliza na Baragumu kwa upande wa maigizo.
IJUMAA: Kwenye maigizo kama Sayari, Taswira na hayo mengine yaliyofuata, akina Kanumba na Ray walikuwemo, lakini si miongoni mwa wasanii uliowakuta Kaole, ni lini walijiunga?


BEN: Alianza Ray kujiunga akitokea Kundi la Nyota Ensemble na baadaye akaja Kanumba, Ray aliwahi kuwamwalimu wa mazoezi pia. Licha ya kujiunga kama msanii wa kawaida, uwezo wake ukaonekana Kanumba alijiunga baadaye akiwa mwanafunzi Kidato cha Tano
IJUMAA: Nini kilifuata baadaye?
BEN: Kwanza nisisahau. Baadaye tuliacha kurusha maigizo yetu ITV, tukahamia TVT kwa sasa TBC1.
IJUMAA: Baada ya Igizo la mwisho la Baragumu, nini kilitokea na kwa nini hilo ndilo lilikuwa igizo la mwisho?
BEN: Wasanii wengi waliamua kubadili aina ya uigizaji na kuamua kujiingiza moja kwa moja kwenye fi lamu, Ray na Kanumba wakajiunga na Kampuni ya Game 1st Tz Limited chini ya Mtitu Game, kisha nami nikaitwa kujiunga nao.
IJUMAA: Ilikuwaje ukaitwa?


BEN: Marehemu Kanumba ndiye alimshawishi Mtitu kuhusu uwezo wangu, akamwambia ukweli kwamba ndiye nilikuwa natunga
maigizo ya Mizengwe. Moja kwa moja nikapewa mkataba na kuanza kutunga maigizo chini ya Mtitu.
IJUMAA: Filamu yako ya kwanza kuigiza ni ipi?
BEN: Inaitwa Chumba Na. 77.
IJUMAA: Ni fi lamu ngapi umecheza kwa Mtitu?
BEN: Nyingi sana, lakini kwa uchache ni kama Dar 2 Lagos, She’s My Sister, Magic House, Unfortunate Love, More Than Pain,Morning Alarm, Fake Smile, Penina na nyingine nyingi.
IJUMAA: Ikawaje baada ya kutoka kwa Mtitu?
BEN: Kanumba alishindwana na Mtitu, akaanzisha kampuni yake ya Kanumba The Great Film, akanichukua na tukaanza na fi lamu ya This Is It na nyingine zilizofuata kama Big Dad, Deception, The Shock na nyingine nyingi.
IJUMAA: Kwa sasa fi lamu za nje zimekamata soko, tumeona hivi karibuni baadhi ya wasanii
wakiandamana, nini kifanyike ili hadhi ya fi lamu zetu irudi?
BEN: Kwanza, hadhi ya fi lamu ipo. Tatizo siyo kuandamana kupinga
uingizwaji wa fi lamu za nje, dawa kubwa ni kuboresha fi lamu zetu, ubunifu uongezeke na serikali iingilie kati kwa kuweka utaratibu maalum wa namna ya kuuza filamu zetu,
IJUMAA: Umeshindwa nini kufanya fi lamu zako mwenyewe?
BEN: Sikutaka kukurupuka, kwa sasa najiandaa kuingiza sokoni fi lamu yangu iitwayo My Car, ambayo iko tofauti sana, chini ya kampuni yangu ya Busy Production.
IJUMAA: Ni mchekeshaji gani unamkubali hapa Bongo?
BEN: Heshima abaki nayo King Majuto. Pia, wapo wengine kama Masanja Mkandamizaji, Joti, Bambo na wengine wengi.
IJUMAA: Ben umezaliwa lini na wapi?
BEN: Nimezaliwa Kigogo jijini Dar (Hospitali ya Muhimbili), mwaka
1983.

Leave A Reply