The House of Favourite Newspapers

Ben Pol: Ustaa ulinifanya niitwe Coke Studio

0

Ben-Pol_full

Mkali wa R&B nchini, Benard Paul ‘Ben Pol.

MKALI wa R&B nchini, Benard Paul ‘Ben Pol’ ameweka wazi sababu za kuitwa kwenye msimu mpya na wa tatu wa Coke Studio uliofanyika nchini Kenya wiki kadhaa zilizopita kuwa ustaa ulichangia kuitwa kwake.

Akizungumza na Risasi Vibes, Ben Pol anayetamba na Wimbo wa Sophia alisema kuwa, hakuwa anajua kama atashiriki msimu huu mpya, lakini alishangaa kupigiwa simu na Coke Studio kisha kuambiwa atakuwa mmoja wapo atakayeiwakilisha Bongo na walifanya hivyo baada ya kumfuatilia kazi zake mitandaoni hususan Mtandao wa Youtube.

“Kwa kiasi kikubwa ustaa wangu umenifanya nishiriki katika msimu huu mpya wa Coke Studio. Namshukuru Mungu muziki wangu kukubalika kila pande kumenifanya nionekane nje ya Tanzania,” alisema Ben Pol.

Msimu mpya wa Coke Studio utaanza kuonekana kwenye TV mbalimbali nchini kuanzia Oktoba 10, mwaka huu huku staa huyo akiwa amefanya ngoma kibao na staa wa muziki nchini Kenya, Wangechi kama vile Sophia, Ningefanyaje na Jikubali.

Leave A Reply