The House of Favourite Newspapers

BENKI YA AZANIA YAJA NA AMSHA NDOTO

Benki ya Azania hivi karibuni imetangaza neema kwa wateja wake kwa kuwaanzishia huduma kampeni ya Amsha Ndoto ambayo itawaingiza kwenye droo maalum ambayo washindi wataibuka na kitita cha milioni tatu kila mwezi.

 

Akizungumza na wanahabari Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Charles Itembe amesema kigezo cha kuingizwa kwenye droo hiyo ni kuwa mteja wao aidha mpya au wa zamani ambaye kwenye akaunti yake ana kiasi kuanzia milioni moja. Mkurugenzi huyo amesema ushindi huo utaweza kumfanya mshindi kuweza kutatua changamoto zake.

Itembe amewahamasisha Watanzania kuwa na utamaduni wa kujiwekea fedha benki ili kujiimarisha kifedha na kuwashauri kutumia huduma zao za akaunti ya kawaida, akaunti ya ziada na akaunti ya watoto.

 

Comments are closed.