KIBIBI APIGA CHINI WASIOJIONGEZA

Mwigizaji anayefanya poa kunako Tamthiliya ya Huba, getrude Richard almaarufu kibibi amesema unapoona una rafiki asiyejiongeza, dawa ni kumpiga chini. Kibibi aliliambia Gazeti la Ijumaa kuwa, maisha ya sasa yamebadilika mno hivyo ni bora kuendana na mtu anayependa maendeleo na si vinginevyo. “Kiukweli kama una rafiki ambaye hana mawazo yoyote chanya ya

maendeleo na kukushauri mambo mazuri kwenye maisha, badala yake ni kupiga tu umbeya, sidhani kama ni rafiki bora wa kuwa naye kwenye maisha,” alisema Kibibi ambaye anatabiriwa kuwa mwigizaji mkali zaidi kwenye Bongo Muvi.


Loading...

Toa comment