The House of Favourite Newspapers

Benki ya DCB Yadhamini Tuzo za Ubora wa Elimu

Waziri katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Suleiman Jaffo, akikabidhi cheti cha shukurani kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa (kushoto), kwa kutambua udhamini wa benki hiyo katika hafla ya kutoa Tuzo za Ubora wa Elimu Tanzania kwa wanafunzi, walimu, shule, halmashauri  na mikoa waliofanya vizuri katika mitihani ya taifa mwaka 2019 iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu Tamisemi, Godfrey Mweli.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mtaa, Joseph Kandege (kulia), akishikana mikono na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa baada ya kupokea cheti cha shukurani kutoka kwa Waziri wa Tamisemi, kutokana na  udhamini wa benki hiyo katika hafla ya kutoa tuzo za Ubora wa Elimu Tanzania  kwa wanafunzi, walimu, shule, halmashauri  na mikoa waliofanya vizuri katika mitihani ya taifa mwaka 2019.
Baadhi ya wanafunzi waliohudhuria hafla ya utoaji tuzo za Ubora wa Elimu Tanzania kwa wanafunzi, walimu, shule, halmashauri  na mikoa waliofanya vizuri katika mitihani ya taifa mwaka 2019 iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wahudhuriaji katika  hafla ya utoaji tuzo za Ubora wa Elimu Tanzania kwa wanafunzi, walimu, shule, halmashauri  na mikoa waliofanya vizuri. 
Ofisa Mahusiano wa Benki ya Biashara ya DCB, Dalila Issa (wa pili kushoto), akitoa maelezo kuhusu  akaunti maalumu ya masuala ya elimu ya DCB Skonga iliyozinduliwa na benki hiyo hivi karibuni wakati hafla ya utoaji tuzo za Ubora wa Elimu Tanzania. 
Mkuu wa Idara ya Wateja Binafsi wa Benki ya Biashara ya DCB, Fredrick Mwakitwange (kushoto), akimfahamisha Angel Lomwai kuhusu faida ya akaunti maalumu ya mpango wa elimu ya ‘DCB Skonga’ iliyozinduliwa na benki hiyo hivi karibuni wakati wa hafla ya utoaji tuzo za Ubora wa Elimu Tanzania kwa wanafunzi, walimu, shule, halmashauri  na mikoa waliofanya vizuri katika mitihani ya taifa mwaka 2019.

Comments are closed.